Ndugu msomaji wa habari hii, kwanza nianze kwa kukusalimia habari za wakati huu.
Ikiwa ni siku chache baada ya kuandika habari iliyokuwa na jina la ''Uchakachuaji wa leseni ndicho chanzo cha ajali za barabarani'' sasa majibu yamejidhilisha wazi siku ya jana mida ya saa saba na dakika hamsini na nne mchana.
Tukio la ajali iliyotokea siku ya jana lili ihusisha gari dogo aina ya cresta pamoja na gari kubwa aina ya scania, maeneo ya Tbc pale Tazara jijini dar es salaam.
Chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dreva wa gari dogo baada ya kulazimisha kupanda ukuta ambao ni mpaka wa barabara kuu na matokeo yake akashindwa kulimudu gari lake kisha akajikuta analigonga ubavuni gari kubwa la mizigo aina ya scania.
Baada ya ajali hiyo kutokea ili wasababishia usumbufu mkubwa watumiaji wengine wa barabara hiyo kwani magari hayakuweza kupishana na matokeo yake yalisababisha foleni ambayo ilianzia eneo hilo la tukio mpaka eneo la supper doll, Ambapo foleni hiyo ilidumu zaidi ya muda wa nusu saa nzima.
Kwa habari za Matukio Kitaifa, Kimataifa, Michezo na Burudani, Ungana nami kupitia Link zifuatazo hapo chini.
In order you follow me just click one of the Icon Button above.