Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

BALOZI WA QATAR AMEAGWA NA WAZIRI BERNARD MEBE LEO

Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,  Mhe. Bernard  K. Membe (Mb.) akimkaribisha ofisini kwake Balozi wa kwanza wa Qatar nchini
Tanzania Mhe. Jassim M. Al-Darwish alipokwenda kumuaga rasmi baada ya kumaliza muda wake wa kazi hapa nchini.



Waziri Membe akizungumza jambo na Balozi Jassim M. Al-Darwish huku Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati Balozi Simba Yahya (kushoto) akisikiliza.

Afisa Mambo ya Nje, Bw. Batholomeo Jungu akisikiliza mazungumzo kati ya Waziri Membe na Balozi Al- Darwish ambao hawapo pichani Hafla ya kumuaga Balozi Al-Darwish.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe (Mb.) akitoa neno la shukrani kwa Balozi wa Quatar Mhe. Jassim M. Al-Darwish, kwenye Hafla ya Chakula cha Mchana iliyoandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje  kwa ajili ya kumuaga Balozi Al-Darwish ambaye amemaliza muda wake wa kazi hapa nchini.


Sehemu ya Wajumbe kutoka Wizara  ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Ubalozi wa Qatar wakati wa hafla ya kumuaga Balozi Al-Darwish.


Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Mindi Kasiga pamoja na wageni wengine waalikwa wakifuatilia hotuba iliyokuwa ikitolewa na Mhe. Membe (hayupo pichani) wakati wa hafla ya kumuaga Balozi Al-Darwish wa Qatar ambaye amemaliza muda wake wa kazi hapa nchini.


Balozi Jassim M. Al-Darwish akitoa hotuba yake wakati wa hafla ya kumuaga ambapo alitoa shukrani kwa Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano aliopata katika kipindi chote alichokuwepo hapa nchini na kuomba ushirikiano huo uendelee.


Sehemu ya Wageni waalikwa wakati wa hafla ya kumuaga Balozi wa Qatar akiwemo Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati, Balozi Simba Yahya (wa pili kulia) wakimsikiliza Balozi huyo (hayupo pichani) alipowahutubia.



Waziri  Membe (Mb.) akimkabidhi zawadi ya picha yenye mchoro wa Tembo  Balozi wa Kwanza wa Quatar nchini Tanzania Mhe.  Al-Darwish wakati wa hafla fupi ya kumuaga Balozi huyo ambaye amemaliza muda wake wa kazi hapa nchini. 

Picha ya Pamoja.
  


Kwa habari za Matukio Kitaifa, Kimataifa, Michezo na Burudani, Ungana nami kupitia Link zifuatazo hapo chini.

    

In order you follow me just click one of the Icon Button above.
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.

Share habari hii kadri uwezavyo.

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top