Jeshi la polisi zanzimbar limeweza kukamata mtu mmoja ambaye alikuwa amebeba mabomu manne ya kivita ambayo yanasadikiwa kuwa ni miongoni mwa mabomu yanayotumika katika vitendo vya uharifu vilivyotokea sehemu mbalimbali hapa nchini.
Kamishina wa jeshi la polisi zanzibar CP Hamdani Omar Makame amethibitisha kukamatwa kwa mtu huyo, ambapo mtu huyo amekiri kuwa anajishugulisha na mtandao wa kuagiza, kuingiza na kuhifadhi mabomu ya kivita ya kurusha kwa mkono.
Kijana huyo mpaka sasa yupo mikononi mwa polisi na sheria zinaendelea kuchukua mkondo wake kwa mujibu wa sheria za nchi na siyo imani za kidini. Wakati polisi imekataa kutoa taarifa yeyote kuhusu mtuhumiwa huyo jeshi hilo limesema hakuna kosa lolote la kisheria endapo mtu akipelekwa nje ya zanzibar kwa kosa la ugaidi, huku akisema bado polisi wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo kama ni la zanzibar au nila mtandao wa ugaidi wa nchi nzima.
Kwa habari za Matukio Kitaifa, Kimataifa, Michezo na Burudani, Ungana nami kupitia Link zifuatazo.
FACEBOOK >>> TWITTER >>> MATUKIO >> MUSIC MPYA