Kundi la kitakfiri la Boko Haram la nchini Nigeria limeendelea kutekeleza jinai baada ya kushambulia kijiji cha Maffa kilichoko katika jimbo la Borno na kuwateka nyara watoto 30.
Alhaji Shettima Maina kiongozi wa kijiji hicho amesema kuwa, watoto hao waliotekwa nyara ambao ni mchanganyiko wa wavulana na wasichana wana umri wa kati ya miaka 11 na 13. Wiki iliyopita, wanamgambo wa Boko Haram walishambulia miji ya Wagga na Gwarta iliyoko kaskazini mashariki mwa Nigeria na kuwateka nyara karibu wanawake 60.
Hivi karibuni Rais Goodluck Jonathan wa Nigeria pamoja na jeshi la nchi hiyo walitangaza kutiwa saini makubaliano ya kuachiliwa huru wanafunzi wasichana wapatao zaidi ya 250, lakini kundi hilo licha ya kukanusha taarifa hizo bado linaendelea kuwateka nyara wananchi wa maeneo ya kaskazini mashariki mwa Nigeria. Wakati huohuo, Wizara ya Ulinzi ya Cameroon imetangaza kuwa, wanajeshi wa nchi hiyo wamefanikiwa kuwauwa wanamgambo 39 wa Boko Haram wakati walipozima mashambulio matatu yaliyofanywa na wanamgambo hao ndani ya ardhi ya Cameroon.
Kundi la Boko Haram licha ya kuwa tishio kwa usalama wa Nigeria, limesababisha kukosekana amani na utulivu katika nchi jirani pia.
Kwa habari za Matukio Kitaifa, Kimataifa, Michezo na Burudani, Ungana nami kupitia Link zifuatazo hapo chini.
In order you follow me just click one of the Icon Button above.