Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

CHANGAMOTO ZINAZOUKUMBA UWANJA WA NDEGE PEMBA

Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.
Uongozi wa uwanja wa ndege Pemba, umeziomba mamlaka husika kuwapatia mashine maalumu za ukaguzi wa mizigo na abiria, ili kuepusha mizigo ya abiria kupekuliwa kwa mikono, kitendo ambacho huwakera abiria.

Akizungumza na mtandao wa Zanzibanews, Meneja wa uwanja huo, Rajab Ali Massoud, alisema tabia ya wafanyakazi wa uwanja huo kupekua mizigo kwa kuifungua, huwaudhi abiria wengi na wakati mwengine kutoa lugha zisizo nzuri.

Alisema kwa sasa wafanyakazi hao huwalazimu kuifungua mizigo ya abiria na kupekua na wakati mwengine husababisha migogoro na abiria.

Alisema wakati umefika kwa serikali kuharakisha ununuzi wa mashine hizo ili kuwa na uhakika wa kile kinachopitishwa badala ya kuangalia mizigo kwa macho na mikono mitupu.

“Hivi sasa wafanyakazi wa uwanja huu wanalazimika kutumia mikono wakati wa kupekua mizigo ya abiria wanaosafiri kwa ndege, lakini tukipata mashine ndio suluhisho,” alisema.

Aidha alisema kuwepo uhaba wa wafanyakazi pamoja na baadhi ya vitendea kazi husababisha kutokufanya kazi zao kwa ufanisi.

Alisema kuanzia mwaka 2013-2014 idadi ya abiria wanaotumia uwanja huo imeongezeka kutokana na safari za ndege kuongezeka.

Mkuu wa ulinzi na usalama,Ali Sudi Ali, alisema ukosefu wa wafanyakazi pamoja na mashine ya kukagulia mizigo ya abiria ni kikwazo katika uwanja huo.

Alisema juhudi za kuiomba serikali zimeshachukuliwa na hivi karibuni wanatarajiwa kupatiwa kifaa hicho lakini ni vyema serikali kuharakisha upatikanaji wa kifaa hicho.
 


Kwa habari za Matukio Kitaifa, Kimataifa, Michezo na Burudani, Ungana nami kupitia Link zifuatazo.

 FACEBOOK >>> TWITTER  >>> MATUKIO >>  MUSIC MPYA
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.

Share habari hii kadri uwezavyo.

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top