Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

BABA MZAZI ADAIWA KUMBAKA MWANAE WA KIKE WA MIAKA 17

Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.
SERIKALI ya Kijiji cha Bwekela,Kitongoji cha Mwina, kata ya Igoweko,wilayani Igunga, Mkoa wa  Tabora inamtafuta mkazi mmoja wa Kijiji hicho, Kashinje Shima kwa tuhuma za kumbaka na kumpa mimba mtoto wake wa kike,Mbalu Kashinde mwenye umri wa miaka 17.

Mama mzazi wa mtoto huyo,Jeni Njiro alisema tukio hilo lilitokea Julai,23,mwaka huu baada ya binti huyo kugundulika kuwa na ujauzito wa miezi saba sasa. Alisema kabla ya kugundua kitendo hicho cha kinyama kilichokuwa kikifanywa na mumewe, inasemekana kuwa baba wa mtoto huyo alikuwa akitumia mwanya wa kutokuwepo nyumbani kwa mama wa mtoto na ndipo alipokuwa akifanya tendo hilo la ndoa na mtoto wake.
Kutokana na hofu aliyoanza kuwa nayo juu ya mwenendo wa mumewe na mtoto wake huyo ndipo siku moja walipokuwa shambani wakiendelea na shughuli za kuvuna mazao na mara tu mumewe alipoaga kurudi nyumbani,muda mfupi baadaye naye alimtuma mtoto wake mkubwa wa kiume ili akafuatilie nyumbani kupata uhakika wa kile alichokuwa akihofia.

Hata hivyo mama huyo alisema mara baada ya mtoto wake huyo kufika nyumbani ndipo alikuta baba yake wakifanya tendo la ndoa na mdogo wake na hivyo kurudi shambani na kumweleza ukweli wa jambo hilo mama yake.

Ndipo inasemekana baada ya taarifa hiyo mama yake aliamua kuita ndugu wa pande zote mbili kwa ajili ya kuzungumzia unyama huo na alipohojiwa katika kikao hicho cha kifamilia, alikana kuhusika na tuhuma hizo,na baada ya babu ya mtoto huyo kushauri waende kupimwa Hospsitali kupata ukweli, ndipo baba huyo alipokubali kuwa anatembea na mtoto wake.

Kutokana na kukubali kwake kwa mume wa mama huyo kwa kuhofia kwenda kugundulika kutokana na vipimo kuonyesha ukweli hivyo alitakiwa kulipa adhabu ya faini ya ng’ombe wawili,ambao aliwalipa na suala hilo kuwa limekwisha. Hata hivyo pamoja na familia ya upande wa mama huyo kutokubaliana na maamuzi hayo ya kifamilia.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kitongoji cha Mwina Bundala  Makelema alikiri kuwepo kwa suala hilo na kwamba wakati  mtuhumiwa huyo akilipa adhabu ya kimila ya ng’ombe wawili yeye alishiriki.

Jiunge na mi kwa kubonyeza kwenye link zifuatazo chini ili kupata habari mpya zaidi. 
          FACEBOOK >>> TWITTER  >>> MATUKIO KWA NJIA YA SAUTI
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.

Share habari hii kadri uwezavyo.

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top