Tanzania imekuwa moja ya nchi nne Afrika iliyotunukiwa tuzo ya kimataifa ya usafiri wa anga duniani na Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga duniani (ICAO) kutokana na mchango wake mkubwa katika ukuaji na usalama wa anga katika bara la Afrika.
Tuzo hiyo ilitolewa hivi karibuni mjini Dakar, Senegal na Rais wa ICAO, Dk. Bernard Aliu katika kikao cha 24 cha Kamisheni ya usafiri wa anga afrika.
Pichani Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania, John Chacha akipokea tuzo hiyo kutoka kwa Rais wa ICAO, Dk. Aliu.
Jiunge na mi kwa kubonyeza kwenye link zifuatazo chini ili kupata habari mpya zaidi.