Ebola ni nini?
Ugonjwa wa Ebola pia hujulikana kama Ebola Haemorgic Fever husababishwa na virusi vya Ebola. Ebola ni jina la mto katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kijiji kimoja kati ya vijiji viwili vya kwanza ugonjwa huo kugundulika ilikuwa eneo hilo mwaka 1976 . Kijiji kingine kilikuwa Sudan. Ebola ni ugonjwa wa hatari sana ambao huanza ghafla baada ya kugusana na wanayama au mizoga katika maeneo ya misitu ya mvua ikiwa ni pamoja na sokwe, nyani, popo, swala na wengine . Ugonjwa huu unaua hadi 90% ya wale ambao wameathirika.
Je huambukizwaje?
Virusi wa Ebola huambukizwa toka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kupitia damu au majimaji mengine ya mwili , lakini pia vitanda, shuka, nguo au vitu vingine vilivyogusana na mgonjwa iwapo vimeguswa. Taratibu za mazishi ambazo uhusisha kugusa mwili pia ni hatari. Virusi huingia mwilini kupitia kwenye vidonda au ngozi nyepesi.
Kundi lililo katika hatari zaidi ni wafanyakazi wa afya, na wale wanaotunza watu walioathirika na Ebola. Wanapaswa kuvaa nguo za kuwakinga mwili mzima ikiwa ni pamoja na mask, miwani ya usalama, na wanapaswa kubadilika mipira ya mikinoni kati ya mgonjwa mmoja na wa pili.
Dalili zake ni zipi?
Dalili za awali ni homa ya ghafla, udhaifu mkali, maumivu ya misuli, kuumwa na kichwa na koo. Dalili hizo hufuatiwa na Kutapika na kuharisha,hivi huongeza hatari ya mgonjwa kumwambukiza mtu mwingine. Figo na ini vinakuwa vimeathirika hivyo magonjwa anaweza kutokwa na damu ndani na nje ya mwili, hii ndio maana ukaitwa Ebola Haemorgic Fever. Wagonjwa huanza kuambukiza mara tu dalili zinapojitokeza, ambayo huwa ni kati ya siku mbili hadi 21 tangu kupata maambukizi.
Matibabu yake ni yapi?
Kuna matibabu kidogo sana. Wagonjwa lazima walazwe katika Chumba cha uangalizi maalum, na matibabu huwa ni kuongezewa maji kwa njia ya mishipa au maji ya chumna au kunywa maji ya chumvi chumvi. Wahudumu pamoja na watu wanaokuja kuwa tazama lazima wavae mavazi ya Kuwakinga mwili mzima Ugonjwa huu hauna tiba wala chanjo . Hata hivyo utafiti unaendelea kutafuta chanjo.
Kwa nini ni hakuna tiba?
Imeonekana kuwa ni vigumu sana kupata madawa ya kutibu magonjwa ya virusi kutoka kwa wanyama, kama homa ya mafua ya ndege na VVU. Ingawa kiwango cha vifo kiko juu, pia milipuko ya ebola imekuwa ikatokea mara chache na yote imekuwa ikidhibitiwa kila wakati. Hakuna soko hivyo uwezekano wa kupata faida ni mdogo makampuni ya madawa yanasita kuwekeza katika utafiti na maendeleo ya dawa za Ebola.
Kwanini unatokea tena baada ya kudhibitiwa?
Ugonjwa huu unaweza kudhibitiwa kwa binadamu lakini si katika hifadhi yake kwa wanyama na popo. Hivyo binadamu anapogusana na mnyama aliyeathirika hupata maambukizi tena.
Jiunge na mi kwa kubonyeza kwenye link zifuatazo chini ili kupata habari mpya zaidi.