Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

WANAWAKE ZAIDI YA 60 WATEKWA NYARA, SOMA ZAIDI

Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.

Wapiganaji wa Boko Haram wanataka kutawala eneo la Kaskazini mwa Nigera kwa kutumia sheria ya kiisilamu. Inaripotiwa kuwa wanawake pamoja na wasichana sitini walitekwa nyara Kaskazini Mashariki mwa Nigeria wiki iliyopita.Ripoti zilizotolewa mwishooni mwa wiki iliyopita zilisema kuwa ishirini kati yao walichukuliwa na kundi linaloaminika kuwa Boko Haram.

Wanawake hao walitekwa wakati wa uvamizi uliofanywa katika vijiji vilivyo katika wilaya ya Damboa katika jimbo la Borno.Wanawake hao inaarifiwa walitekwa nyara katika eneo la vijijini ambakop mawasiliano ni magumu sana , sababu ya kupata habari hizi kuchelewa. Watu wanaotoroka vijiji ambavyo vilishambuliwa, wanasema kuwa wanawake na wasichana sitini walitekwa nyara wiki jana.

Baadhi ya watoto waliotekwa ni wadogo sana wa umri. Moja ya vijiji vilivyoshambuliwa ni kile cha Kummabza kilicho katika eneo la Damboa katika jimbo la Borno. Hata hivyo haijaweza kuthibitisha idadi kamili ya watu waliotekwa nyara. Hali hii imefanywa kuwa ngumu'kwani maafisa wa eneo hilo bado hawajatoa tamko lolote kuhusu kisa hiki labda kutokana na hofu juu ya maisha yao.
Serikali ya Nigeria imekuwa ikishinikizwa kuwanusuru waliotekwa nyara eneo la Chibok, Sio jambo la kushangaza kwamba tangu kutekwa nyara kwa wasichana miambili wa shule kutoka Chibok , wanawake wengine wametekwa nyara. Vijiji vingi katika eneo la Kaskazini mwa Nigeria, vinakumbwa na utovu wa usalama na wakati ambapo Boko Haram wanapofanya shambulizi,wao huchukua muda mrefu wakifanya uporaji na mauaji.

Mwishoni mwa wiki, idadi kubwa ya watu waliuawa karibu na eneo la Chibok.
Zaidi ya wasichana 200 wa shule walitekwa nyara eneo la Chibok mwezi Aprili
Walitekwa nyara kutoka shule yao ya mabweni na wapiganaji wa Boko Haram.
Serikali ya Nigeria imekuwa chini ya shinikizo kali za kuitaka ifanye jitihada za kuwaokoa wasichana hao.
Jiunge na mi kwa kubonyeza kwenye link zifuatazo chini ili kupata habari mpya zaidi. 

             FACEBOOK >>> TWITTER  >>> MATUKIO KWA NJIA YA SAUTI
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.

Share habari hii kadri uwezavyo.

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top