Shirika la Afya Duniani (WHO) limetahadharisha juu ya uwezekano wa kuenea ugonjwa wa Ebola barani Afrika. Msemaji wa WHO ameeleza kuwa, mlipuko wa ugonjwa wa Ebola magharibi mwa Afrika ambao kwa mara ya kwanza ulishuhudiwa katika mipaka ya nchi 3 za eneo hilo, unaripotiwa kuwa uliyakumba maeneo mengi zaidi kijiografia toka ugonjwa huo ugunduliwe.
Ameongeza kuwa, mlipuko huo haujaisha na kwamba kila siku kesi mpya zinaripotiwa nchini Guinea, Sierra Leone na Liberia, kwa ajili hiyo nchi nyingine zinatakiwa kuchukua tahadhari.
Wakati huo huo Jumuiya ya Madaktari Wasio na Mpaka imetangaza kuwa, mlipuko wa Ebola katika nchi za Guinea, Sierra Leone na Liberia haudhibitiki na kwamba kuna hatari ya kuenea katika maeneo mengine.
WHO imetangaza kuwa, ugonjwa huo umesababisha vifo vya watu 566 katika nchi hizo 3 tangu ulipoanza huko Conakry mji mkuu wa Guinea. Dalili za homa ya Ebola ni kuhara na kutapika sambamba na homa kali ambayo pia huandamana na uvujaji mkubwa wa damu. Homa ya Ebola huambukizwa kwa kugusa damu, jasho na kinyesi cha mtu mwenye ugonjwa huo.
Pia tunapatikana FACEBOOK TWITTER NA MATUKIO KWA NJIA YA SAUTI