Mtu mmoja ambaye amefahamika kwa jina la Joseph Admin mwenye umli wa miaka 35 mkazi wa kijiji cha Matundasi wilaya ya Chunya, aliuwawa kwa kupigwa sehemu mbalimbali za mwili wake na kundi la wananchi walioamua kujichukulia hatua mkononi wakitumia siraha za jadi zikiwemo fimbo, mawe, marungu nk.
Tukio hilo limetokea jana majira ya saa nne usiku, katika ofisi ya kijiji cha matundasi,kata ya matundasi tarafa ya kiwanja wilaya ya chunya.
Kundi hilo la wananchi likiongozwa na Fabiani John na Thobias Asukenye, walivunja walivunja mlango wa ofisi iyo, na kuanza kumshambulia marehemu ambaye alikuwa amekamatwa pamoja na mwenzake akitambulika kwa jina la Abbas Jumanne mwenye umli wa miaka 29, kwa tuhuma ya kuiba ving'amuzi viwili vya kampuni ya Star Times chunya mjini ambavyo walikutwa navyo.
Baada ya kutoa taarifa kituo cha polisi, ndipo polisi waliweza kufika kwenye eneo la tukio. Polisi walifanikiwa kumuokoa Abbas Jumanne, wakati watuhumiwa wengine kama Fabian John na Thomas Asukenye wakikimbia na wenzao wengine walioshiriki katika mauaji hayo.
Bado polisi inawatafuta kuwakamata ili waweze kueleza kwa kile walicho kifanya.