KIBAKA APEWA KIPONDO MPAKA ASEMA BASI YATOSHA.
Kumekuwa na matukio kadhaa ya kusikitisha yanayoendelea kutokea hapa nchini na sehemu nyingine za dunia, lakini moja kati ya vitu ambavyo vimeshika kasi kwa sasa hapa nchini ni swala la wananchi kujichukulia sheria mkononi pale yanapokuwa yametokea matukio ya kiuharifu mfano kupiga watu wanaodhaniwa kufanya uharifu huo mpaka kuwauwa kitu ambacho usababisha kupoteza ushaidi.
Picha unayoiona hapo juu ni moja kati ya vijana ambao walidhaniwa kumkwapua mkoba dada mmoja na wananchi wakaanza kumwaadhibu. Ndugu msomaji wangu, kama ulisahau ule usemi usemao kwamba, ukimchekea nyani utavua mabua, sasa naomba leo ukaukumbuke maana atawewe kama ukimchekea mwizi siku moja atakuja kukuliza. Kwaiyo tusaidiane kupinga tabia ya mwizi kwenye maeneo yetu tunayo ishi, ata kama ni maeneo ya kazini, pamoja na sehemu nyingine.