HII NDIYO HIFADHI YA TAIFA MKOANI ARUSHA.
Hifadhi ya Arusha inapatikana katika mji wa Arusha nchini Tanzania. Hifadhi hii ina ukubwa wa kilometa za mraba 542, iko umbali wa kilometa 32 kutoka katika mji wa kitalii wa Arusha.
Maeneo makubwa na ya muhimu ya hifadhi hii ni Bonde la Ngurdoto(Ngurdoto crater) pamoja na Maziwa ya Mamella ambayo kila moja hutoa mandhari tofauti pamoja na Mlima Meru wenye urefu wa meta 4566 ambazo ni sawana futi 14990 hali inayofanya hifadhi kuwa na mazingira ya baridi na yenye kupendeza sana siku zote.
Hifadhi hii ni maarufu kwa wanyama wenye jamii ya tumbili wajulikanao kama Mbega weusi na weupe. Wanyama wengine wanaopatikana kwa wingi katika hifadhi hii ni pamoja na Twiga, Pundamilia, Nyati na Digidigi. Aidha unaweza kuwaona baadhi ya wanyama kama Chui wakibarizi katika vivuli vya matawi ya miti inayokingwa na maanguko ya maji huku makundi kadhaa ya Batamaji yakitafuta wadudu katika maziwa ya Momella.
Zaidi ya aina 400 za ndege wamethibitika kupatikana ndani ya hifadhi hii. Mambo yanayoweza kufanyika ndani ya hifadhi hii ni pamoja na kufanya utarii kwanjia ya Safari za miguu na kupanda mlima Meru ni moja ya burudani muhimu katika hifadhi hii. na mpandaji anahitaji siku 3-4 za kupanda mlima. Wakati mzuri wa kutembelea hifadhi hii ni kati ya mwezi Juni na Februari ingawa mvua inaweza kunyesha mwezi novemba. Na hii ndio hifadhi ya taifa iliyoko mkoani Arusha.