Wakati
asili inapoongezeka, matokeo yake huwa mabaya sana kilimwengu na
husababisha matatizo makubwa; nyumba huharibiwa, miji hupoteza hadhi
yake, na maisha ya watu wasiokuwa na idadi hupotea. Hii ni juu ya watu
kujenga upya miji yao, sanjari na misaada ya kiutu kutoka katika Jamii
ya Kimataifa. Lakini bara la Afrika limekubwa na machungu makubwa sana
ya majanga ya asili ukilinganisha na sehemu nyingine.
Makala haya yanakusudia kuangaza majanga ya asili mabaya zaidi kuwahi kutokea katika historia ya bara la Afrika.
Njaa ya Ethiopia, 1983-1985
Inakadiriwa kuwa watu 400,000 walipoteza maisha yao Kaskazini mwa Ethiopia pekee katika janga hilo la njaa ambalo lilisababishwa na ukame ulioikumba nchi hiyo katika miaka ya mwanzo ya 1980. Kwa ujumla upande wa Kaskazini, uhaba wa mvua ulisababisha ekari myimhi za mazao kufa katika mashamba ya wakulima, hata ikapelekea kukosekana chakula nchi nzima. Hali hii ilisababishwa pia na Serikali kutokuwa imara pamoja na rushwa, na uwepo wa makundi ambayo yalikuwa kikwazo kwa misaada ya kimataifa kuwafikia walengwa.
Mlipuko wa Nabro, 2011
Juni 12, 2011, volacano ya Nabro ambayo inapatikana katika mpaka wa nchi za Eritrea na Ethiopia ililipuka bila ishara zozote za tahadhari kwa mara ya kwanza katika historia iliyorekodiwa. Zaidi ya watu 30 walipoteza maisha katika mlipuko huo, na maelfu zaidi wakakosa makazi yao baada ya kuharibiwa vibaya na miji yao. Pia watu zaidi ya 10,000 waliathirika kutokana na wingu zito ambalo lilikuwa ni matokeo ya sulfur dioxide kutoka ardhini na baadhi yao waliathirika zaidi baada ya misaada kuchelewa kuwafikia.
Kimbunga Leon-Eline
Mwezi Februari 2000, kimbunga Leon-Eline cha nguvu kilitokea katika Bahari ya Hindi na kushambulia nchi za Mozambique na Madagascar huku ikiacha athari kubwa kwa kuwafikia zaidi ya watu 1,000, na zaidi ya watu 300,000 walipoteza makazi yao na miji ikafurika maji. Nchini Mozambique, hali hii ilikuwa hatari zaidi baada ya nchi hiyo kuwa katika kipindi cha kukaa sawa kufuatia Cyclone Connie kuikumba nchi mapema mwaka huo. Athari pia zilifika nchini Afrika Kusini ambako kulishuhudia mvua kubwa hata kusababisha mafuriko pia.
Ukame wa Afrika Mashariki, 2011
Katika kile kinachotajwa kuwa ni "Ukame mbaya" kwa miongo kadhaa, pembe ya Afrika na Somalia kwa ujumla ilikuwa katika hali ngumu karibia mwaka mzima kuanzia Julai 2011. Matokeo yake ni uhaba wa chakula ambao ulisababisha mazao kufa na mifugo kupotea ambapo inakadiriwa kuwa watu 12.4 milioni kutoka nchi za Kenya, Somalia, Ethiopia, na Djibouti waliathirika. Umoja wa Mataifa ulitoa misaada ya kiutu, lakini mwitiko mdogo ulisababishwa na shughuli za kijeshi na mazingira hatarishi katika eneo husika. Janga la wakambizi likaongezeka na mamia ya maelfu ya wanawake na watoto walihamia katika nchi za jirani wakikimbia vita vya kisiasa na njaa Kusini mwa Somalia.
Mafuriko ya Mozambique, 2000
Katika miezi ya Februari na Machi 2000, nchi ya Mozambique ilishuhudia mvua kubwa kuwahi kutokea katika historia ya karibuni ya nchi hiyo; mvua hiyo ilidumu kwa zaidi ya wiki tano bila kukoma. Watu wanaokadiriwa kufika 800 walipoteza maisha katika mafuriko na zaidi ya maelfu waliathirika baada ya makazi yao kuharibiwa vibaya na mifugo kufa. Inakadiriwa kuwa mifugo 20,000 ilipotea, sanjari na kilomita elfu nyingi za mashamba kuharibika. Zaidi ya watu 44,000 waliwachwa bila makazi wakati mvua hiyo ilipofikia ukomo, na Serikali ikajitahidi kutafuta misaada kwa ajili ya waathirika hao.
Tetemeko la ardhi la Crete 365 AD
Wakati ni ngumu kuweza kukisia ama kutathimini uharibifu uliosababishwa na tetemeko la ardhi 365 AD mjini Crete, inadhaniwa kwamba maelfu ya watu walipoteza maisha katika nchi zilizokumbwa na tatizo hilo, ikiwemo maeneo ya Afrika Kaskazini hasa katika nchi za Misri na Libya. Tsunami ambayo ilifuatia tetemeko iliharibu miji na vijiji Kaskazini mwa Libya na mji wa Alexandria, na ukanda wa Nile Delta uliathirika — ardhi, makazi, na maisha ya watu yalipotea.
Mafuriko ya Afrika Kusini, 2010-2011
Ikianzia Desemba 2010, mvua kubwa ilisababishwa na tukio la La NiƱa nchini Afrika Kusini ilisababisha zaidi ya dola za kimarekani 200 milioni kupotea. Watu wapatao 141 walipoteza maisha yao na zaidi ya Kanda 30 za hatari zilitangazwa na Serikali ya Afrika Kusini katika majimbo manane miongoni mwa majimbo tisa ya nchi hiyo. KwaZulu Natal ndiko hasa kuliharibiwa sana, na maelfu ya wakazi wake waliondolewa baada ya makazi yao kuharibiwa na mvua na kufurika mito.
Kimbunga Kamisy, 1984
Aprila 9-10, 1984, kimbunga kibaya cha kitropiki kiliikumba Madagascar kuwahi kutokea katika karne za hivi karibuni na kusababisha maporomoko katika sehemu za Kaskazini za nchi jirani na Diego Suarez. Janga la nchi nzima, kimbunga Kamisy kilikuwa na upepo uliokwenda kasi ya 160 kwa saa na kudondosha mvua kubwa. Karibu watu 100,000 waliwachwa bila makazi ikiwa ni matokeo ya kimbunga, na vifo 68 viliripotiwa. Majiji na miji katika sehemu za Kaskazini iliharibiwa na inakadiriwa kuwa dola 250 milioni zilitumika.
Tetemeko la ardhi la Agadir, 1960
Februari 29, 1960, tetemeko la ardhi la kipimo cha a 5.7-magnitude lilitokea katika mji wa bandari wa Agadir, Morocco, likasababisha uharibifu mkubwa katika mji huo na sehemu za jirani. Licha ya kuwa lilichukuliwa kama matetemeko mengine lakini zaidi ya watu 12,000 walipoteza maisha na wengine karibu 40,000 walijeruhiwa au kupoteza makazi yao. Wataalamu walisema kuwa miundombinu mibovu katika mji wa Agadir ilisababisha athari zaidi. Tetemeko hilo linachukuliwa kuwa mbaya zaidi katika historia ya Morocco ambalo liliigharimu nchi hiyo mamilioni ya dola kuujenga tena mji huo.
Tetemeko la ardhi la Toro, 1966
Wakati matetemeko mengine yaliyopita hayakuwa na uharibifu mkubwa barani Afrika na sehemu nyingine za dunia, tetemeko la Toro 1966 lilikuwa na athari sana katika nchi za Uganda na Jamhuri ya Kidemkrasia ya Kongo. Machi 20, 1966, tetemeko la ardhi lenye kipimo cha a 6.8-magnitude lilitokea katika mpaka wa nchi mbili, ingawa inaweza pia kudhaniwa kupita katika nchi za Tanzania, Rwanda, Burundi, na Kenya. Zaidi ya watu 150 walipoteza maisha katika tetemeko hilo, lakini wengine 100 walifariki miezi iliyofuata ktuokana na mshtuko (wengi walifariki Mei 18 mwaka huo). Majengo yalianguka, na makazi yakaharibiwa.
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies