Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana amesema, hoja zilizoshawishi marekebisho ya kumi ya Katiba ya Zanzibar hazikuwa na mashiko ya kujenga utaifa, badala yake zilikuwa na sababu za kuleta mpasuko usiokuwa na tija kwa Watanzania.
Akizungumza katika mahojiano na gazeti hili, Kinana alisema marekebisho hayo yaliyoitambua Zanzibar kuwa nchi, ni makosa ambayo pande zote mbili za Muungano zinatakiwa kuyajutia kwa kukosa umakini na kuhisi kuwa ongezeko la mambo ni kuzikandamiza.
Kwa mujibu wa marekebisho hayo, Zanzibar ilitambuliwa kuwa nchi na kumpokonya mamlaka ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika ugawaji wa mikoa na wilaya kisiwani humo, na kumpa mamlaka hayo Rais wa Zanzibar.
Alifafanua kuwa baada ya kuvunjika kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki mwaka 1977, sehemu zote mbili za Muungano hazikuona ukweli ni upi mpaka kufikia muundo ulioleta mgogoro wa kikatiba mpaka sasa.
Alisema sababu nyingine ya kufanya marekebisho hayo ni pamoja na msukumo wa kisiasa kutoka kwa vyama vya upinzani.
Kinana alionya kuhusu mgawanyiko, akisema: “Ni vyema tukakumbuka athari za Uzanzibari na Uzanzibara zilizoelezwa na Mwalimu Julius Nyerere.” alisema.
Azidi kumpinga WariobaKinana aliendelea kupingana na mapendekezo ya muundo wa Serikali tatu ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyoongozwa na Jaji Joseph Warioba, akisisitiza kuwa waziri huyo mkuu wa zamani anatakiwa kutoa ufafanuzi kuhusu hoja zilizofichika.
Hata hivyo, Jaji Warioba alipohojiwa na kuhusu madai hayo alisema: “Nisingependa kuzungumzia tena suala hilo kwa sababu nilishaeleza kila kitu bungeni.