Wakazi wa eneo la Kongowe katika Manispaa ya Temeke, wameliomba shirika linalo jihusisha na ujenzi wa barabara nchini Tanzania Tanroads.
Wakazi hao lawama zao zilizo nyingi ni juu ya uwekaji vituo vya kupakia na kushushia abilia katika maeneo yao.
Wanaendelea kwa kusema kwamba, tangu barabara iwepo katika eneo lao hawana vituo maalumu vya kupakia na kushushia abilia, zaiddi ya kuwa na kituo kimoja tu, ambacho kinaudumia wasafili wanao toka Mbagala to kongowe, au Kongowe to Temeke.
Kitendo hicho kimekuwa chanzo kikubwa sana cha ajari zisizo kuwa na maana katika eneo hilo, kutokana na madereva wa magari makubwa pamoja na daradara kupaki ovyo kando ya barabara ili kushusha abilia wao.
Kwaiyo tulikuwa tunaiomba wizara husika ikasikie kilio chetu ili tuondokane na adha hii tunayo ipata katika eneo letu hili.
Pia tunahitaji barabara hii ikawekewe matuta katika eneo la kanisa pamoja na eneo la kituo cha mafuta Oilcom kongowe ili kunusuru maisha ya wanafunzi pamoja na watu wengine kwa ujumla, wanao tumia eneo hilo kuvuka kutoka eneo moja na kuelekea eneo lingine.