Kwanza kabisa Nnaanza kwa kuwasalimu wote mabibi na mabwana,
Asalaam Aleykum,
Tumsifu Yesu Kristo,
Bwana Yesu Asifiwe.
Asalaam Aleykum,
Tumsifu Yesu Kristo,
Bwana Yesu Asifiwe.
Poleni kwa majukumu yetu ya kila siku ya kutafuta riziki,na ujenzi wa taifa letu.Kwa sasa kuna wamiliki wa mitandao ya kijamii (Blogs) isiyopungua 50,000+ hapa kwetu nchini Tanzania.
Hivyo mojawapo ya sifa ya uandishi hasa kwa wana habari ni ubunifu.Ninaamini kwamba hapo ulipo sipo ulipohitaji kuwepo miaka mitano iliyopita au miaka mitano ijayo kwani yawezekana wewe au mimi tunaweza kufanikiwa zaidi.
Swali: Je,Ni mara ngapi tunapata kipato kutokana na Blog Zetu Hizi?Kwa kulifikiria hilo tumeona ni vyema kutumia mitandao yetu ya kijamii kujiingizia kipato,kwani tunatumia mitandao hii kupashana habari kama jukumu kuu,lakini pia ni vyema tujitahidi iwe kama ajira rasmi ya kujiajiri kwani katika nchi zilizoendelea kila kitu kinatumika kuingiza fedha za kuendesha maisha yako ya kila siku.
Tafadhali kama una malengo ya mafanikio zaidi ya haya uliyo nayo kwa kutumia blogu yako,usikose kikao kifupi tarehe 12/4/2014 kuanzia saa nane kamili mchana katika hoteli ya Holiday Inn mtaa wa azikiwe jijini Dar es salaam kwani tutapeana fursa ambayo itakuwa mojawapo ya njia ya kuingiza kipato kwa kutumia mtandao wako wa kijamii (Blog) unaomiliki.
Imetolewa na Mr.Khushe.M. Hauli
(Mwezeshaji) 0784-488 488
(Mwezeshaji) 0784-488 488