Hapa ni kwenye makutano ya barabara ya Mandela na ile barabara iendayo Mwembe hanga. ikiwa ni mida ya saa nane mchana wa leo ndipo tukio hili limetokea katika maeneo haya.
Eneo hili linafahamika kwa jina maarufu sana kama Vetinali, ambapo eneo hili liko karibu sana na wizara ya kilimo.
Huyu mwenye mwavuli, ni moja kati ya mashahidi ambao wameshuhudia tukio zima la ajari hiyo, kwa jina anaitwa Bonge (jina la kazi), akiwa anaenda kuwapatia taarifa kamili traffic juu ya tukio lilivyo tokea.
Kwa mujibu wa bwana bonge amesema, "Gari lenye namba T434 ASK, mali ya mwanajeshi, lilikuwa kwenye service road likitokea maeneo ya wizara ya kilimo kilielekea Sokota, liliferi break na kuingia ubavuni mwa roli la mizigo".
Hawa ni moja kati ya mashuhuda wa tukio hili, wakiendelea kushilikiana na traffic katika ukamilishaji wa taarifa juu ya tukio hili.
Wakati kwa upande wa pili likiwepo gari lenye namba za usajili T279 BRH, linalofanya safari zake za Temeke To Ubungo, likiwa nalo limepata ajari baada ya kuchanwa ubavuni na gari la kushusha mizigo.