Wakazi wa maeneo ya (TIA) maarufu kama uhasibu pamoja na maeneo yote ya Mbagala, wametoa malalamiko yao juu ya shirika la umeme nchini Tanzania Tanesco kwa kukatiwa umeme bila ya taarifa yeyote ile.
Kwa taarifa zilizo tufikia kutoka kwa wakazi hao nikwamba, mnamo tarehe 26/3/2014 majira ya saa 11:59 usiku, wakati mvua inaanza kunyesha tu, ghafla umeme ulikatika, jambo ambalo nikawaida umeme kukatika nyakati zamvua.
Lakini jambo la kushangaza mpaka leo hii yapata siku ya pili hatuna umeme kabisa. Wala hakuna taarifa zozote zile ambazo zimetoka tanesco kuhusu swala hili, swali je shirika la umeme tanzania Tanesco, hamna taarifa juu ya swala hili? Na je kama mnazo taarifa nini hatima yake?
Lakini kwa upande wa pili wa shilingi wakazi jiji la dar es salaam waishio mabondeni khali zao nitete kwa sababu ya kuhofia usalama wa maisha pamoja na mali zao kwa ujumla.