Wafanyakazi walioajiriwa na shirika la Reli Tanzania (TRL) wakitoa mchanga kwenye kichwa cha treni ya mizigo kilichopata ajali usiku wa kuamkia katika stesheni ya Gulwe, Wilaya ya Mpwampwa mkoani Dodoma.
Katika ajali hiyo watu wawili wamefariki dunia na wengine saba kujeruhiwa na kulazwa katika hospital ya Benjamin Mkapa Wilayani Mpwampwa.
Sehemu ya mabehewa ya mafuta na ngano ambayo hayakusombwa na maji katika ajali iliyotokea usiku wa kuamkia leo katika stesheni ya Gulwe, hiyo imetokea saa 9.15 usiku.
Treni hiyo ya Mizigo ilikuwa ikitokea Dar es Salaam na kuelekea Mkoani Kigoma na ilikuwa na mabehewa yaliyobeba ngano, sukari na mafuta.
Njia ya Reli iliyoondolewa na maji katika stesheni ya Gulwe Wilaya ya Mpwampwa kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha maeneno mbambali nchini ndicho chanzo cha ajari hiyo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Shaaban Mwinjaka akitoka kwenye maji baada ya kuangalia kichwa cha treni kilichopata ajali na kusombwa na maji katika stesheni ya Gulwe, Wilaya ya Mpwampwa, usiku wa kuamkia leo, (hayupo kwenye picha).