Mashabiki wa AC Milan waja na staili mpya ya kukaa uwanjani…unajua kwa sababu gani? Michezo Kutofanya vizuri kwa klabu ya AC Milan kumewafanya mashabiki wao kuingiwa na hofu na uongozi uliopo madarakani hadi kufikia hatua ya kuandamana.
Mmiliki wa klabu hiyo Silvio Berlusconi ambaye ameiongoza klabu hiyo kwa miaka zaidi ya 30 ameonekana kuchokwa na mashabiki wa timu hiyo ambao sasa wameamua kuandamana kutaka aondolewe kwenye nafasi yake.
Mashabiki hao wameandamana kwa staili ya aina yake huku wakikaa uwanjani na kuonesha alama ya ‘BASTA’ ikimaanisha “Sasa imetosha”. Wengi wanataka kiongozi huyo aiuze klabu yake ili mtu mwingine atakayeinunua ifanye vizuri.
Kwa habari za Matukio Kitaifa, Kimataifa, Michezo na Burudani, Ungana nami kupitia Link zifuatazo hapo chini.
In order you follow me just click one of the Icon Button above.