WAWEZA KUJITIBU ALLERGY KWA KUTUMIA MAJI YA KUNYWA
Katika makala hii tutajifunza mengi kuhusu Aleji au mzio kwa Kiswahili zaidi. Tutaona uhusiano uliopo baina ya upungufu wa maji mwilini na ugonjwa wa aleji na ikiwa utanielewa basi utakuwa umeelewa namna ya kujikinga au kujitibu na ugonjwa huu ambao unasumbua watu wengi sana.
Mwaka 2006 mpaka 2007 nilikuwa nikisumbuliwa sana na aleji ya vumbi. Wakati huo nikipita barabara ya vumbi ilikuwa lazima nijifunike pua maana kama gari ingepita karibu na kunitimulia vumbi basi ningepiga sana chafya na hata kukohoa, lakini nilipojuwa uhusiano wa aleji na upungufu wa maji mwilini na kuanza kuyanywa ndipo nilipoona kitu kigeni kinatokea.
Ni kuwa ndani ya mwezi mmoja tu tangu nianze kuifuatilia tiba kwa kutumia maji basi aleji hiyo ya vumbi ilipotea kiasi kwamba hata ukitupa vumbi moja kwa moja kuja usoni kwangu hakuna chochote ambacho kinatokea iwe ni chafya au kikohozi. Aleji katika lugha nyepesi kabisa ni kitendo cha mwili kupungukiwa maji wakati histamini inapozarishwa kupita wastani ili kuhimiza unywaji wa maji na ugawanywaji wa kiasi kidogo cha maji kipatikanacho mwilini.
Histamini ni kihisio cha kwanza (primary sensor) cha ubongo kinachozarishwa ili kujishughurisha na ugawanywaji wa maji kwa viungo mhimu wakati kunapokuwa na upungufu wa maji mwilini. Inajihusisha na kazi ya ugawanywaji wa kiasi kidogo kinachopatikana cha maji (maji ya mgawo kutokana na wewe kuendelea kusubiri kiu ndipo unywe maji) wakati wa upungufu wa maji mwilini (Unintentional chronic dehydration).
Histamini katika lugha rahisi:
Histamini ni kemikali ambayo miili yetu huitoa inapohitaji msaada kusawazisha upungufu wa vitu mhimu sana mwilini kama maji, chumvi au potasiamu. Histamini na wasaidizi wake wengine watano (5 buddies) watasaidia kuusawazisha upya mwili ambao upo nje ya usawa. Kwa hakika Histamini ni kitu kizuri ambacho huokoa maisha yetu kwa mujibu wa Dr. Batmanghelidj.
Sababu ya kutokuelewa namna hasa histamini inavyofanya kazi mwilini, dawa zimetengenezwa kuidhiti. Wakati histamini imezarishwa, yaweza kuendelea kuzarishwa na kuzarishwa kwa sababu tunakula au kunywa kitu kimoja ambacho miili yetu haiwezi kukitumia. Mfano mzuri ni juisi ya chungwa. Juisi ya chungwa huwa na kiasi kingi cha potasiamu ambayo miili yetu haiwezi kuitumia bila uwepo wa chumvi.
Kwahiyo, inapotokea mtu anakunywa juisi ya chungwa na hatumii kiasi kinachostaili cha chumvi ili kuiwezesha potasiamu kuziingia seli za mwili, basi histamini hutolewa kurekebisha tatizo hilo. Kila mtu anahitaji 3/4 gramu za chumvi kwa kila 250 ml za juisi ya chungwa ili potasiamu iliyomo kwenye chungwa iweze kutumika na seli za mwili.
Katika kitabu kiitwacho‘’ABC of Asthma, Allergies and Lupus’ kilichoandikwa na Dr. Batmanghelidj , ukurasa wa 149 chini na juu ya ukurasa wa 150, Dr. Batmanghelidj ameandika: “Ni sera nzuri kuongeza kiasi cha chumvi katika juisi ya chungwa ili kusawazisha matendo ya sodiamu na potasiamu katika kuhimili ujazo unaotakiwa wa maji ndani na nje ya seli.”
Katika baadhi ya tamaduni, chumvi huongezwa katika matikiti na matunda mengine ili kukazia utamu wa matunda hayo. Kwa ujumla, matunda haya mengi huwa na potasiamu tu kwa sehemu kubwa. Kwa kuongeza chumvi kabla ya kuyala, usawa kati ya uchukuwaji wa sodiamu na potasiamu hupatikana. Jambo hili lapaswa kufanyika pia kwa matunda mengine. Ni mhimu pia kuongeza kiasi kidogo cha chumvi katika juisi unayotengeneza nyumbani na hata katika keki.
Kile ulikuwa hujuwi labda hadi sasa ni kuwa tunahitaji chumvi kwa kila tunachokula kwa sababu ya potasiamu. Potasiamu inapatikana karibu katika kila kitu tunachokula. Ndiyo, CHUMVI yaweza kuwa MBAYA kwetu ikiwa hatunywi maji ya kutosha kila siku ili kusawazisha ulaji huo mwingi wa chumvi.
Moja kati ya matatizo makubwa siku hizi ni kuwa watu hatunywi maji ya kutosha. Badala yake tumehamia kwa kahawa, chai, soda, pombe na kadharika. Mwili wa binadamu unahitaji maji halisi na chumvi. Uthibitisho wa hili ni matumizi ya madripu ya maji chumvi (SALINE IV’s) katika mahospitali na magari ya kukimbizia wagonjwa mahututi (ambulances).
Madaktari kamwe hawampi mgonjwa dripu la maji matupu, bali lenye chumvi ndani yake. Lita moja ya dripu la maji huwa na chumvi gramu 9. Ukiwa mahututi katika ambulance hupewi kahawa, Madaktari watakutundikia dripu la maji chumvi na wakati mwingine watakutundikia lita nyingine ya vitamini, madini au dripu la maji sukari (dextrose or glucose).
Mdhibiti mzuri kabisa dhidi ya histamini ni chumvi. Ikiwa unakunywa maji mengi kila siku na hautumii chumvi ya kutosha katika vyakula unavyokula au hata kuitafuna chumvi yenyewe kwa ajili ya maji hayo mengi unayokunywa, mwili utaizarisha tena histamini. Unaweza kulithibitisha hili wakati unapopatwa ghafla na chafya kubwa, au kujisikia kama koo linaziba hivi na msongamano katika pua au koo kwa ujumla. Ikiwa unalazimika kukohoa (au kubanja) ili kusafisha koo lako kila mara, ni ishara unapungukiwa chumvi mwilini.
Hali hii pia hutokea wakati tunakula vyakula au kunywa vinywaji vyenye potasiamu nyingi (hivi mara nyingi ni vile vyakula vya kwenye makopo au maboksi vya madukani) na bila kutumia chumvi nyingi kwa ajili ya potasiamu ya kwenye vyakula au vinywaji hivyo. Utapata chafya kubwa na ya ghafla au kujisikia msongamano katika mapafu au koo lako. Chumvi nyingi kuzidi pia itasababisha kuzarishwa kwa histamini na utapatwa na chafya ya ghafla, msongamano mapafuni au kooni kama ilivyofafanuliwa hapo juu. Macho ya mtu yaweza pia kuonesha wakati histamini imezarishwa mwilini kwa kutoa maji maji (runny eye).
Unapokunywa maji na unapatwa na dalili mojawapo kama hizo hapo juu, basi utatakiwa kuweka kiasi cha chumvi katika ulimi wako na dalili zinapaswa kuwa zinapotea. Ikiwa unakula chakula na ukapatwa na dalili mojawapo hapo juu, utahitaji chumvi zaidi kwa ajili ya potasiamu. Weka tu kipande cha chumvi mwanzoni mwa ulimi wako na ikiwa dalili hizo (kupiga chafya kubwa, msongamano kooni au mapafuni au kwikwi) zinatulia, utathibitisha kuwa unachokisoma hapa ni sahihi. Kujaribu hakuwezi kumuumiza mtu.
Hauhitaji kumeza chumvi, iache tu kama vile unavyomung’unya pipi juu ya ulimi wako kwa dakika moja au mbili na kisha unaweza kuisafisha na maji kwenda chini au iteme na uiweke pembeni. Histamini ni nini? ((medical): Histamine is a chemical substance that is given out in the body in response to an injury or an allergy – Oxford Advanced Learners Dictionary 8th edition).
Ikiwa umetumia chumvi kuzidi au umeweka chumvi juu ya ulimi na ukapatwa na dalili mojawapo hapo juu, basi utakunywa kikombe kimoja cha maji au viwili na dalili zinapaswa kuwa zinatoweka. Kila mmoja anahitaji kuzijua ishara zake na kujaribu kupata usawa mahususi wa maji kwa chumvi vivyo hivyo kwa kiasi mahususi cha chumvi kwa chakula anachokula. Mdhibiti mwingine mkuu kabisa tuliye naye mwilini mwetu dhidi ya histamini ni adrenalini. Adrenalini hutolewa na mojawapo ya tezi mbili za adreno (adrenal grands) zipatikanazo juu ya figo.
Kahawa au kafeina, ndicho kitu kinachoweza kuisisimuwa tezi ya adreno kuitoa adrenalini. Kaffeina pia itasababisha mwili kuitumia hifadhi yake ya nguvu ambayo mwili huihitaji wakati wa kushughurikia matendo ya dharura (emergency). Ikiwa hifadhi ya nguvu ya dharura inatolewa wakati hakuna udharura, mwili utajikopa wenyewe kile unachokihitaji wakati wa dharura na hivyo kujihakikishia uwezo wakati wa dharura nyingine.
Kaffeina itapelekea mwili kujila au kujitafuna wenyewe (cannibalize off itself). Kila seli ndani ya mwili inahitaji maji na chumvi ili ziwe seli zenye afya ambazo zitafanya kazi pamoja kumuweka mtu katika afya bora. Kusoma mengi kuhusu kaffeina yaani kwamba kaffeina ni nini na inapatikana katika nini na namna ambavyo unaweza ukawa unaitumia kila siku pasipo wewe mwenyewe kujuwa, bonyeza hapa => goo.gl/002p4T
Matumizi ya vidhibiti vya histamini vya kibiashara, yataendelea kuuacha tu mwili na upungufu wa maji na chumvi. Hebu fikiri tu kwanini madaktari wanatuambia tuwe mbali na chumvi na sodiamu kwa sababu si vitu vizuri kwetu. Madaktari wanasema tunapata chumvi nyingi kuzidi katika vyakula vyetu siku hizi. Muombe Daktari au muuguzi wako akuelezee kwanini wanatoa madripu ya maji chumvi kwa wagonjwa mahututi wakati wanakuambia unapata chumvi nyingi kuzidi katika chakula chako siku hizi?.
Tatizo letu siku hizi hatunywi tena maji halisi ya kutosha. Tumegeukia vinywaji vya kibiashara. Wanyama katika bustani za wanyama hunywa maji halisi na wakati mwingine husafiri umbali mrefu zaidi kutafuta tu maji. Mbwa na paka wengi hawapati chumvi ya kutosha siku hizi ndiyo maana ukimsogelea mbwa au paka cha kwanza atataka kukulamba ngozi yako, ni kwa sababu ya chumvi iliyo juu ya ngozi yako. Inashauriwa uongeze kiasi cha chumvi katika maji yao unayowapa kunywa na utaona mabadiliko makubwa kwa wanyama wako.
Kwanini mwili unapatwa na aleji au mzio?:
Histamini ni kemikali wakala wa ubongo mwenye kazi dhidi ya bakteria, virusi na mfumo wakinga ya mwili dhidi ya maadui wa nje, kwa kuongezea inajihusisha pia na kazi ya ugawanywaji wa maji mwilini. Wakati wa kiasi cha kawaida cha maji mwilini, yaani unapokuwa unakunywa maji ya kutosha kila siku, shughuli hizi (za kumonita bakteria, virusi, kinga ya mwili na usambazaji maji) zinabaki tulivu au hazitengenezwi. Wakati upungufu wa maji (dehydration) unapobaki kwa muda mrefu, Ubongo unaamuru uzarishwaji mwingi wa histamini kuvutia uchukuaji wa maji.
Mfumo huu wa histamini wenye seli utazarisha kiasi kingi cha transimita nyurolojia (neurotransmitters). Ni kitendo hiki cha uzarishwaji mwingi wa histamini kinachotoa picha au majibu kuwa una Aleji katika maabara. Aleji inapaswa kutibiwa na ongezeko la kiasi cha unywaji maji. Kwa wastani hali hizi zinapotea baada ya siku tatu hadi wiki nne za urekebishwaji wa ongezeko la unywaji maji.
Uzarishwaji wa histamini utapunguwa wenyewe kwa ongezeko la unywaji maji.
Kitu kingine mhimu wakati unaendelea kuyarudishia maji taratibu mwilini mara baada ya kukutwa una Aleji ni vitamin C. Ni mhimu kutumia vyakula, matunda, mboga za majani na juisi zenye vitamin c kwa wingi na hapa napendekeza juisi ya ubuyu, kitunguu swaumu, unga wa mlonge na matunda karibu aina zote. Ni kwa sababu vitendo vile viletwavyo na aleji huathiri pia kinga ya mwili kwa kiasi kikubwa sana.
Kwa habari za Matukio Kitaifa, Kimataifa, Michezo na Burudani, Ungana nami kupitia Link zifuatazo hapo chini.
In order you follow me just click one of the Icon Button above.