Ilikuwa mida ya saa sita na nusu mchana wa leo, katikati ya eneo la Msikitini na Mission hapa Mbagara.
Gari ambalo sikuweza kupata namba yake ya usajiri, ambayo ni Scania iliyokuw imebeba mborea aina ya Urea, iliweza kupata ajari kisha kumwaga mborea hiyo barabarani mchana wa leo.
Hapo chini ni moja ya gari ambalo lilikuwa limebeba mborea hiyo.
Baada ya gari kupata ajali vijana waishio katika maeneo hayo ya msikitini pamoja na Mission ndipo walianza kujichukulia mborea hiyo.
Pichani hapo juu wanao onekana ni wakazi wa maeneo hayo wakiendelea kujizolea mborea iliyokuwa imemwagika kandokando ya barabara kwa ajili ya kujipatia kipato.
Kipindi chote hicho ambacho vijana hao walikuwa wakiendelea kujichukulia mborea hiyo aina ya urea, nikipindi ambacho polisi walikuwa hawajafika kwenye eneo la tukio, lakini pia baada ya police kuwasili kwenye eneo hilo vijana hao waliendelea na zoezi lao kama kawaida tena bila ya uoga.
Na hapa ndipo police walikuwa wamewasili kwenye eneo la tukio kwa ajiri ya kuimalisha ulinzi pamoja na usalama.
Kwa habari za Matukio Kitaifa, Kimataifa, Michezo na Burudani, Ungana nami kupitia Link zifuatazo hapo chini.
In order you follow me just click one of the Icon Button above.