Katika hali isiyokuwa ya kawaida leo asubuhi nyumbani kwa mhe.Diwani wa kata ya sinza Renatus Pamba, pametokea mdudu wa maajabu ambaye ni kwa mara chache sana huonekana mududu huyo ajulikanaye kama Kakakuona, watalaamu wa mambo ya kimira na watu wa kale wanasema Mdudu huyo akionekana mahali popote huashilia neema na faraja kubwa kwa mwaka huo au mwaka ujao.
Ila maswali ya kujiuliza je kwa nini atokee nyumbani kwa diwani ikizingatiwa kuwa pale alipo diwani amezungukwa na nyumba nyingi kwa nini haikuwa katka moja ya nyumba za majirani zake?
Asubuhi ya leo wazee wa mambo ya kale walifika nyumbani kwa mhe.Diwani wakamwekea vitu mbali mbali vikiwemo mikuki majembe na Nk, lakini cha ajabu mdudu huyo hakwenda hata sehemu mojawapo ila zaidi alikuwa akimkimbilia mhe. diwani na kuingia kila chumba cha nyumba yake na kutoka sebuleni kwake.
Wazee wakamshauli diwani yeye ajaribu kumpatia kile anachofikili kwa maana anaonekana ni mgeni wa diwani moja kwa moja. Diwani akampatia maji akaenda akaanza kuyalamba, akampatia pesa elf kumi akaenda kuinusa na kuitemea mate, akampatia maziwa akayalamba.
Vitu vingine nimeombwa nisiviandike hadharani kwani ni siri za ndani kwa familia yake na mambo yake ya kisiasa Kakakuona huyo kamwekea alama ya vema hasa alipompa kitabu cha kanuni za bunge na bendera ya CHADEMA alivikimbilia vyote, Haikupatikana bendera ya CCM kwa haraka. Je unalipi la kumwambia diwani kwa hichi kitendo cha kihistoria?
Kwa habari za Matukio Kitaifa, Kimataifa, Michezo na Burudani, Ungana nami kupitia Link zifuatazo hapo chini.
In order you follow me just click one of the Icon Button above.