Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

MSANII JOSEPH OLITA WA UGANDA AFARIKI DUNIA

Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.
Wakati Tanzania tukiendelea kuwa na majozi ya vifo 3 mfululizo kutoka kwenye tasnia ya filamu Tanzania,wenzetu nao Uganda wamempoteza jamaa aliyeigiza kama Idi Amini,Idi Amini wengi wanamfahamu kutokana na matukio mengi aliyowahi kufanya ingawa kuna kizazi hakikuwahi kumuona.

Kupitia filamu ya  The Rise and Fall of Idi Amin,jamaa alicheza kama Idi Amini  na filamu hii ilikua ikielezea matukio yote aliyowahi kuyafanya Idi Amini enzi za uhai wake.


Joseph Olita ambaye ndiye aliyecheza kama Idi Amini amefariki jumapili ya June 01 akiwa na umri wa miaka 70 kusini mashariki mwa Alego huko kogelo Nchini Kenya na ilikua baada ya kumaliza mazishi ya mama yake mzazi.

Mmoja wa ndugu wa Joseph,Bi.Risper Odero amesema kifo cha Joseph Olita kimetokana na shinikizo la damu iliyosababishwa na shughuli nyingi na majonzi wakati wa kumuaga marehemu mama yake mzazi.

Bi Odero amesema kifo cha Olita ni pigo kwa familia hiyo hasa baada ya kumuaga mama yao mzazi masaa kadha kabla ya kifo cha olita,Olita alikua anafanana sana na aliyekua kiongozi wa kiimla Uganda bwana Idi Amin Dada.

Miongoni mwa vitu walivyokuwa wanafanana ni pamoja urefu wa futi sita nchi 5.5 na uzito wa kilogramu 150 na ndiyo maumbile pekee yaliyo wafanya wengi kudhani kuwa olita alikua ndiye Idi Amin.

Mbali na filamu ya The Rise and Fall of Idi Amin ya miaka ya 80 iliyobeba maisha ya Idi Amin kama kiongozi wa kimila aliyeingia madarakani mwaka wa 1971 na kutolewa mwaka 1979 pia ameigiza kwenye filamu ya Mississippi Masala mwaka 1991 na amewahi kuigiza kama polisi kwenye filamu ya Sheena ya mwaka 1984.

Jiunge na mi kwa kubonyeza kwenye link zifuatazo chini ili kupata habari mpya zaidi. 
        FACEBOOK >>> TWITTER  >>> MATUKIO KWA NJIA YA SAUTI
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.

Share habari hii kadri uwezavyo.

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top