Jeshi la nchini Nigeria limesema linajua mahali walikofichwa zaidi ya wasichana 200 waliotekwa wakiwa shuleni lakini hawawezi kuitaja sehemu hiyo hadharani.
Wasichana hao walitekwa na kundi la kigaidi la Boko Haram ambalo linadai haliwezi kuwaachia hadi watakapobadilishana wafungwa wao na serikali ya nchi hiyo.
Kwenye kituo cha TV cha Nigeria, imetangazwa kwamba japo imefahamika walipo Wasichana hao ambao bado wanashikiliwa mateka majeshi ya Nigeria na mengine yanayoendesha opareshen hiyo hayatotumia nguvu za kijeshi kwenye uokoaji wa wasichana hawa.
Kitendo cha kutekwa kwa wasichana hao kimeibua majonzi makubwa miongoni mwa wazazi na kufanya kuibuka kwa kampeni iliyosambaa katika mitandao ya kijamii na vyombo vya habari yenye jina la Bring Back Our Girls ikimaanisha.