Ndege ya Malaysia iliyopotea siku 14 zilizopita, inasadikika kuwa imeanguka kwenye bahari ya Hindi.
wafanya utafiti kutoka mataifa mbali mbali duniani likiwemo taifa la Italy, jana walitoa report zao kuhusu majibu ya upotevu na utafutaji wa ndege hiyo na kusema kwamba, vipimo vyao ikiwemo satelite nk, vinaonesha kwamba ndege hiyo ya malaysia inasadikika kuwa imeanguka ndani ya bahari ya hindi.
Ndege hii ya malaysia inasadikika kupoteza mawasiliano pindi ilipofika katika eneo linalo onekana hapo chini kwenye ramani.
Baada ya kuanza uchunguzi wa ndege hiyo, ndipo walipo baini kuwa ndege iyo inasadikika kuwa katika eneo hili, kama ramani inavyo onesha hapo chini.
pia wataaramu hao wanaendelea kwa kusema kwamba wamebaini mabaki ya ndege hiyo ndani ya bahari ya hindi, ambapo vipimo vinaonesha kwamba kutoka umbali wa mabaki hayo mpaka usawa wa bahari ni umbali wa 2,260KM.
Ifuatayo ni picha ya satelite ambayo inaonesha mabaki hayo ya ndege ya malaysia, kama jinsi inavyo onekana hapo kwenye picha hapo chini.
Lakini mbali na uwasilishaji wa report hiyo, bado tafiti za uchunguzi wa ndege hiyo bado unaendelea mpaka pale watakapo toa final report.