Mchungaji mmoja huko nchini marekani afariki dunia. Ni baada ya kung'atwa na nyoka na kisha akapoteza maisha yake. Habari za kushangaza juu ya mchungaji huyo ni kwamba, katika kanisa lake watu waga wana abudu na kusifu uku wakiwa wameshikilia nyoka mikononi mwao, uku wakiamini ya kwamba binadamu yeyote yule hawezi kung'atwa na nyoka wakati akiwa anaomba wala akisifu maana anakuwa yuko karibu sana na Mungu muumba mbingu na aridhi.
atapia endapo ikitokea nyoka akakung'ata hakuna haja ya kutumia dawa ya kuondoa sumu ya nyoka huyo ndani ya mwili wako, kwa sababu Mungu anakuwa yuko ndani yako wewe muumini au mfuasi wa kanisa ilo. Jamani ama kweli dunia imeisha ndugu zangu, sasa ona Mungu ameamua kuanza na mchungaji, kisha ataendeleza mashambulizi mpaka kwa wafuasi au waumini wa kanisa ilo, na Mungu ameamua kufanya ivyo baada ya kukasilishwa na vitendo tunavyo vifanya sisi wanadamu, kiukweli inasikitisha sana ndugu zangu, ebu tuachane na mambo ya kidunia kisha tupige magoti tusali na kumuomba Mungu wetu atusamehe kwa makosa yetu tunayo mtendea kila siku.