Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

KAHAWA NI DAWA YA MOYO.

Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.
Mbali na faida kemkem tunazozijua zinazopatikana kwenye kahawa, utafiti mpya umebaini na kusema kwamba kunywa kikombe kimoja tu cha kahawa kwa siku kunapunguza hatari ya kupatwa na mshituko wa moyo. 

Utafiti huo uliotolewa katika Kongamano la Jumuiya ya Mshituko wa Moyo la Kimataifa nchini Marekani, umeeleza kwamba kunywa kikombe kimoja tu cha kahawa ya kawaida na isiyokuwa na kafeini kila siku huzuia kupatwa na mshituko wa moyo kwa asilimia 30. 

Hata hivyo wataalamu wameonya kuwa kutumia sana kinywaji hicho matokeo yake huweza kuwa kinyume. Tafiti za huko nyuma pia zilionyesha kuwa, kunywa kila siku kahawa kunaweza kumzuia mtu asipate kisukari aina ya pili na ugonjwa wa akili.

Ndugu mdau baada ya kufahamu hayo, nimeona nichukue fursa hii kuelezea baadhi ya faida za kahawa. Mbali ya kawaha kuwa kinywaji murua ambacho kinaweza kukufanya uchangamke asubuhi baada ya kuamka, au kwa wale kina yakhe wanaopenda kuburudika kwa kunywa kahawa kwa kashata vijiweni au kando ya barabara huku wakipiga story, kinywaji hicho kina faida kemkem kiafya

1. Wataalamu wa Chuo Kikuu cha Tiba cha Harvard cha Marekani wamegundua kuwa kunywa kahawa kunazuia kupatwa na ugonjwa wa kibofu nyongo (gall bladder) au kuzuia mawe katika nyongo (gall stones).

2. Kahawa inazuia kupatwa na ugonjwa wa Alzheimer au kusahau hasa uzeeni.

3. Kahawa ina anti-oxidants ambazo hupambana na seli ambaya zinazosabisha saratani.

4. Kahawa uchangamsha tumbo na kulifanya lifanye kazi vyema na kuzuia matatizo ya kukosa choo. (Bowel stimulant and a laxative). 

5. Kahawa huongeza uwezo wa ufahamu wa akili.

6. Kahawa huuzuia ugonjwa wa figo. 

7. Kahawa pia huzuia ugonjwa wa uvimbe wa viungo hasa mikononi na miguuni.
Lakini wataalamu wanatutahadharisha kwamba ingawa kunywa kahawa kuna faida nyingi kama tulivyoona hapo juu lakini haifai kunywa kahawa kwa wingi kila siku. Kwani kila kitu kinachotumiwa sana badala ya kuwa na faida kinaweza kutuletea madhara.

Sio vibaya kujua kwamba mmea wa kahawa ambayo ni maarufu uliwenguni kote uligunduliwa mara ya kwanza katika nchi za Yemen, Saudi Arabia na kaskazini mashariki mwa Ethiopia na kwa mara ya kwanza zao hilo lilikuwa likilimwa na kutumiwa sana katika nchi za Kiarabu.
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.

Share habari hii kadri uwezavyo.

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top