MAKALA
Daraja la Mandela; Kivutio kikuu Johannesburg
KWA UFUPI
Likiwa na urefu wa mita 248, daraja hilo linapamba anga la Johannesburg kwa rangi za upinde wa mvua hasa nyakati za usiku.
Jo’burg, Afrika Kusini. Tangu kuanza kuumwa kwa Nelson Mandela, watu mbalimbali wamekuwa wakifuatilia mambo mbalimbali yanayohusu maisha yake, mambo yote aliyoyafanya.
Jo’burg, Afrika Kusini. Tangu kuanza kuumwa kwa Nelson Mandela, watu mbalimbali wamekuwa wakifuatilia mambo mbalimbali yanayohusu maisha yake, mambo yote aliyoyafanya.
Wapo wengine wanaofuatilia kwa karibu hali yake kiafya, ingawa hofu imekuwa maisha nchini humo baada ya kifo chake.
Hata hivyo, miongoni mwa vivutio vikubwa ni Daraja la Nelson Mandela jijini Johannesburg.
Hili ni daraja kubwa ambalo lilikamilika kujengwa mwaka 2003, lakini kwa sasa limegeuka kivutio kwa maelfu ya wageni na wenyeji wanaolitembelea, kupiga picha za ukumbusho.
Likiwa na urefu wa mita 248, daraja hilo linapamba anga la Johannesburg kwa rangi za upinde wa mvua hasa nyakati za usiku.
Kwa ufupi, daraja hilo linatumika juu ya njia ya reli inayounganisha vitongoji vya Newtown na Braamfontein, jirani na eneo maarufu la kibiashara lililogharimu Rand 38-milioni.
Wabunifu wake walitaka kuongeza kitu katika uzuri wa jiji hilo la kisasa, kupendezesha eneo la katikati ya jiji hili kwa kulipa sura ya kuvutia.
Lengo lake likiwa ni kuunganisha kitongoji kinachokua cha Newtown na eneo la kibiashara la Braamfontein, pia kuwezesha kuyafikia maeneo hayo kwa urahisi wakati wote.
Ujenzi wake mwanzoni ulionekana kuwa changamoto kubwa kwa timu ya wabunifu na wahandisi wake kupita eneo ambako njia 42 za reli zinapishana bila kuingilia usafiri au kusababisha misongamano ya magari.
Kwa jumla, daraja hilo la Mandela ambalo ni ubunifu wa Kampuni ya Dissing & Weitling, ndilo kubwa la waya Kusini mwa Afrika.
Liliandaliwa maalumu kuwa jepesi, likichanganya vyuma na vifaa vingine vya kuliwezesha kuwa jepesi kwa kadri inavyowezekana, lakini lenye nguvu ya kutosha.
Kulingana na mtandao wa Engineering News, kiasi cha mita za mraba 4,000 za zege, tani 1,000 za vyuma zilitumika kwenye ujenzi wake na tani 500 zaidi ya vyuma maalumu vya kushikilia msingi wake.