Watanzania tumekuwa na tabia ya kila kitu kuilalamikia mamlaka usika.lakini vitu vingine ebu tujiulize,izo mamlaka tunazo zitupia izo lawama je wanafanya mangapi ambayo hatuyasifii?
napenda nitoe mfano mmoja wa awa akina mama ambao wanafanya biashara kando kando ya barabara,wao wafanya biashara katika eneo husika kisha wanaondika pasipo kupafanyia usafi.ila kesho ukifika tena katika eneo ilo ilo,utawakuta wakiwa wanaendelea na kazi zao uku eneo ilo likiwa nichafu,na ukuiliza utajibiwa ivi:
"watu wa jiji/manispaa hawaji kufanya usafi katika eneo letu" je ayo niyakweli ndugu zanguni? ebu angalieni picha apo chini mkajionee wenyewe,ilo nieneo ambalo wakina mama uwa wanafanyia kazi kila siku ya Mungu.na wanapata liziki mungu ana wajalia je kwanini wasilifanyie eneo lao linalo waingizia kipato usafi?
jiji au manispaa wameweka sehemu za kuifadhi takataka je wangapi wanazitumia?
karibu ndugu uchangie mada hii, waweza kuwa na mtazamo tofauti juu ya yaliyo zungumzwa.
KARIBU SANA MDAU WETU.

1 maoni:
Jukumu la Kusafisha maeneo tunayoishi na kufanyia kazi ni letu sisi wenyewe wananchi,hata huko nje mfano us ukipita maeneo mengi utaona ni masafi majani yanayoizunguka nyumba yamekatawa kimpangilio kila nyumba kiasi kwamba wewe mwenyewe unaona aibu kuacha kukata majani nyumbani kwako kwani majirani zako wote utakuta wamekata na kusafisha vizuri,na yote hayo hayafanywi na serikali bali wakazi wa maeneo wenyewe japo kodi wanalipa lakini linakwenda kufanya mambo mengine ya maana si kusafisha maeneo yenye wakazi.
Reply