Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

MANENO YA RAIS KIKWETE JUU YA KULINDA KURA VITUONI

Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.

Rais Jakaya Kikwete amesema watu wanaopanga kubaki katika vituo vya kupigia kura baada ya

Rais Jakaya Kikwete amesema watu wanaopanga kubaki katika vituo vya kupigia kura baada ya kumaliza zoezi hilo kwa lengo la kulinda kura kunaashiria uvunjaji amani, hivyo serikali imejipanga kupambana na hali hiyo siku ya uchaguzi.

Rais amesisitiza kwamba wanaopaswa kulinda kura ni mawakala pekee na si wafuasi wa mgombea ama vyama.

Akizungumza leo katika sherehe za Kilele cha Mwenge wa Uhuru zilizofanyika  Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma, kiongozi huyo anayemalizia muda wake madarakani amesema viongozi wanaowaagiza wafuasi wao kulinda kura wana nia mbaya dhidi ya amani ya nchi.

“Mnatakiwa muondoke kwenye vituo baada ya kupiga kura….kura utazilindaje? Mawakala ndio pekee wanaoweza kulinda. Mkikaidi hilo, hatutawavulimia. Serikali imejipanga kupambana na wale wote watakaokaidi agizo la Tume ya Uchaguzi (NEC),” amesisitiza Rais Jakaya Kikwete.

Katika shehere hizo za mwenge zinazoendana sambamba na maadhimisho ya siku ya kumuenzi Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, Rais Kikwete amewataka Watanzania kuchagua watu waadilifu ambao dhamira ya kupambana na rushwa kwa vitendo.

“Tumchague mtu ambaye hana ukabila, udini na ubaguzi wa rangi…tumchague kiongozi atakayetetea maslahi ya makabila yote 126,” amesema rais huku akimnukuu Mwalimu Nyerere aliyefariki miaka 16 iliyopita.

Sherehe hiyo imehudhuriwa pia na Spika wa Bunge anayemaliza muda wake, Anne Makinda, wakuu wa mikoa na viongozi wengine wa ngazi tofauti serikali na kupambwa na nyimbo za makabila na wanafunzi wa shule mbalimbali mjini Dodoma.
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.

Share habari hii kadri uwezavyo.

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top