Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

WATOTO ZAIDI YA 800 KUKOSA HAKI ZAO NCHINI TANZANIA.

Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.
Ripoti ya Kituo cha Sheria na Haki za binadamu nchini Tanzania imesema watoto wapatao 800 walilawitiwa nchini humo mwaka 2013.


Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika hilo kumekuwa na ongezeko kubwa la vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto nchini Tanzania ambapo kumi kati yao wakiwa wamefanyiwa ukatili huo na wazazi wao wenyewe.

Mwandishi wa BBC Baruan Muhuza anasema ripoti hiyo ya haki za binadamu kwa mwaka 2013 iliyotolewa mjini Dar es Salaam, imebainisha hayo kutokana na utafiti uliofanywa na Kituo hicho cha sheria na Haki za binadamu -LHRC kwa pamoja na kituo cha huduma za sheria Zanzibar.


Akiongea na BBC Mkurugenzi mtendaji wa taasisi hiyo Dr Helen Kijo-Bisimba, amesema watoto wamekuwa katika maisha ya hatari Zaidi nchini humo kutokana na watu wa karibu wakiwemo wazazi wa kiume na hata kaka na wajomba zao kubainika wanawafanyia vitendo vya ubakaji.

Ripoti hiyo ambayo ni ya 11 kutolewa na taasisi hiyo imebainisha kuwepo kwa matukio ya raia kuwaua raia wenzao ambayo yameongeza kasi za ukiukwaji wa haki za kuishi nchini humo.

Aidha utafiti huo umeonyesha kuwa watu zaidi ya 1600 wakiwemo askari polisi wanane, waliuawa na wananchi wenye hasira kali katika matukio tofauti, huku askari polisi nao waliwaua raia 28 katika kipindi cha mwaka 2013.
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.

Share habari hii kadri uwezavyo.

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top