Dawa zifuatazo zimefutiwa usajili na shilika la chakula na dawa TFDA Tanzania.
1. Dawa ya Fungus ya vidonge Ketoconazole inasababisha madhara kwenye ini(Hepatotoxicity)
2. Dawa ya maji ya malaria Amodiaquine-ikitumika peke yake inaleta usugu wa vimelea vya malaria (Drug resistance)
3. Dawa ya maji ya kutibu mafua na kikohozi aina ya PHENYLPROPANOL AMINE inaleta madhara hatarishi kama kiharusi(Haemorrhagic stroke)
4. Antibiotic ya sindano Chlorampenicol Sodium Succinate ya India pamoja na Cloxacillin capsule zinasababisha shida ya kupumua na kupoteza fahamu.