Serikali imewaagiza wafugaji waliovamia maeneo yaliyohifadhiwa ikiwemo hifadhi za taifa,mapori ya akiba na misitu ya hifadhi ya vyanzo vya maji kote nchini kuiondoa mifugo yao kwenye maeneo hayo haraka inavyowezekana kabla nguvun haijatumika kuwaondoa wavamizi hao.
Agizo hilo limetolewa Mjini Morogoro na Waziri wa Maliasili na Utalii ,Profesa JUMANNE MAGHEMBE baada ya kutembelea maeneo na taasisi za uhifadhi za Mkoani Morogoro.
Amesisitiza kuwa kuendelea kupeleka mifugo kwenye maeneo yaliyohifadhiw a na yenye wanyamapori kuna atha ri kubwa kwa uhifadhi wa vyanzo vya maji na kunaihatarisha mifugo hiyo kukumbwa na magonjwa ya wanyamapori ambayo yataifanya nyama ya ng'ombe wa Tanzania isifae kwa matumizi ya binadamu kwenye soko la kimataifa .
Akiwa Mjini Morogoro Profesa MAGHEMBE ametembelea taasisi ya utafiti wa misitu , mfuko wa kuhifadhi misitu ya tao la Mashariki na msitu wa Hifadhi wa Morogoro na akapata taarifa kutoka kwa watendaji wakuu wa taasisi hizo kuwa maeneo mengi ya uhifadhi yanakabiliwa na matatizo mengi ikiwemo uvamizi wa wafugaji ambao wanachunga mifugo katika maeneo hayo kinyume cha sheria .