Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.
Mkuu wa wilaya ya Mkoa Hemed Suleiman Abdalla, amewataka waandishi wa habari Kisiwani Pemba, kuendelea kufuata miiko, na maadili ya kazi yao, ili kuepuka kunyooshewa vidole na kuonekana chanzo kikubwa cha migogoro mbali mbali kwa jamii na taifa kwa ujumla.
Hayo aliyasema jana Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC, tawi la Pemba , wakati alipokuwa akifungua mafunzo ya siku mbili, kwa waandishi hao juu ya ufahamu wa haki za binaadamu na chimbuko lake.
Alisema kuwa ipo haja kubwa kwa waandishi hao, kutosahau kufuata maadili ya kazi zao wakati wanapotafuta, wanapochapisha na kutangaaza habari katika vyombo vyao, ili isiwe ndio chanzo cha migogoro kwa jamii na taifa kwa ujumla.
Alisema kuwa mwandishi mwandishi ni vyema kuhakikisha kwamba anakwenda sawa na maadili ya tasnia hiyo, kwani umuhimu wa mwandishi wa habari katika jamii ni kuhakikisha kwamba anafanya kazi zake ipasavyo bila ya kukiuka sheria za nchi na kuweza kuifikishia ujumbe husika kwa jamii.
“Mwandishi wa mwandishi ni lazima kuifuata miiko yake ya kiuandishi kama inavyotakiwa, kazi zisifanywe kinyume na maadili ya uandishi ,tukifahamu kwamba, tasnia hii ni nguzo muhimu sana kwa jamii”, alisema Hemed alisema.
Aidha Mkuu huyo wa wilaya ya Mkoani Hemed Suleiman, alifahamisha kuwa mwandishi wa habari ndio kioo cha taifa katika jamii , chenye mwangaza mkali unaweza kumwilika mbali kwa lengo la kuibua changamoto ambazo zinawakabili wananjamii, kwa lengo la kuleta mabadiliko ya kimaendeleo ndani ya nchi na taifa kwa ujumla.
Mapema Mratibu wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar (ZLSC) Ofisi ya Pemba, Fatma Hemed Khamis, alifahamisha kuwa lengo la kuwapatia waandishi wa habari mafunzo mbali mbali, ikiwemo ya Haki za Binaadam ni kuona kwamba ipo haja kwa waandishi hao kufahamu na kuyajua majukumu yao katika utekelezaji.
Mratibu huyo aliwataka waandishi hao kupeana mashirikiano katika tasnia hiyo husuani juu ya suala zima la kuzijua haki za binaadamu, ili waweze kufanya haki zao kwa urahisi, kwa lengo la kuleta maendeleo kwa jamii na taifa kwa ujumla.
Akiwasilisha mada inayohusiana na chimbuko, pamoja na historia ya Hakai za Binaadamu, wakili wa serikali Ali Haidar Mohamed, alisema kuwa, chimbuko la haki za binaadamu linatokana na maumbile ya mwanaadamu mwenyewe ambapo linatokana na Mwenyezi Mungu (S.W.) ili aweze kupata haki zake za msingi.
Mwandishi wa habari wa kutoka ZBC- TV, Nasra Mohamed Khatib akiwasilisha wa mada ya kanuni, maadili, na miiko ya waandishi wa habari, alisema kuwa sekta ya habari iliandaa kanuni hizo ili kuondosha migogogro kati yao na Jamii iliyowazunguka.
Nae Mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari Pemba, ‘PPC’ Pemba Khatib Juma Mjaja akiwasilisha mada juu ya Uhuru wa Waandishi wa Habari pamoja na changamoto zinazowakabili, alieleza kuwa miongoni mwa changamoto hizo ni pamoja na waandishi wa habari na vyombo vyao kushindwa kuripoti matokeo mbali mbali hususan wakati wa uchaguzi.
Washiriki hao waliuhakikishia Uongozi wa Kituo hicho kuwa watayafanyia kazi mafunzo hayo ambayo wamewapatia na watahakikisha kwamba watawafikishia na waandishi wengine ambao hawakuhudhuria katika mafunzo hayo, ili lengo la mafunzo hayo liweze kufikiwa.
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.
Share habari hii kadri uwezavyo.