Ndivyo Yanavyoitwa sehemu Mbali Mbali ni Matunda ya asili ambayo kwa Mbayo miti yake inafanana na Mnazi kwa kiasi kikubwa na tunda lenyewe kw haraka linafanana na dafu.
Matunda haya yanapatikana sana Sinyanga, Kahama, Maeneo mbali mbali ya mkoa wa Tabora kama vile kule Nzega Kijiji cha Mwanhala, Kigoma, Singida maeneo ya Iramba, Ikungi na kwingine. Nadhani yawezekana Simiyu, Geita kwa mgawanyo wa mikoa wa sasa.
Ni matunda matamu sana kasoro ndogo ya matunda haya ni kwamba yana harufu nzuri inayopitiliza. Mwanza unaweza kuliogopa lakini ukilionja hutapenda kuacha kulila. Nililazimika kusimama Ikungi Singida kuyaangalia na nikanunua kwenda kuyajaribu. Nashukuru wadau mbali mbali Hapa FB na Sehemu zingine walionijuza zaidi kuhusu matunda haya.
Ni wakati sasa wa Serikali kuwa na Mpango maalumu juu ya matunda ya asili yaweze kuwa na soko. hii itasaidia mambo makubwa mawili, 1. kuwapatia kipato wananchi lakini 2. itasaidia utunzaji wa mazingira maana mimea hiyo itakuwa na msaada mkubwa zaidi wa kiuchumi kwa wananchi.
Kwa habari za Matukio Kitaifa, Kimataifa, Michezo na Burudani, Ungana nami kupitia Link zifuatazo hapo chini.
In order you follow me just click one of the Icon Button above.