Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

SARAFU YA NCHI YA ZAMBIA YASHUKA THAMANI

Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.

Zambia inatafuta msaada kutoka kwa Shirika la Fedha Duniani IMF, baada ya sarafu yake Kwacha, kupoteza thamani yake na bei ya kuuza nje bidhaa zake muhimu za shaba kushuka, shirika hilo limesema, Kuporomoka kwa hivi karibuni kwa thamani ya Kwacha kunaongeza shinikizo la mfumuko wa bei na sera ya kukuza uchumi na fedha imesababisha kwa kiasi kikubwa kukosekana kwa usawa wa bajeti, imeeleza taarifa ya shirika la fedha baada ya ziara na timu ya wataalam wake nchini humo.

Pesa ya Zambia kwacha 500
Mamlaka nchini Zambia imeiomba timu ya IMF kurudi nchini humo mapema mwezi Septemba kujadili mpango wa kiuchumi ambao unaweza kuungwa mkono na shirika hilo. Kwacha imeshuka kwa asilimia 18 katika kipindi cha nusu mwaka uliopita, na kusababisha mfumuko wa bei kuongezeka katika taifa hilo la pili kwa uzalishaji wa shaba barani Afrika.

Pamoja na kushuka kwa bei ya mauzo ya bidhaa yake muhimu ya shaba nje ya nchi, hilo limefanya huduma ya kulipia madeni yake ya nje kuwa na gharama kubwa zaidi kwa serikali.

Zambia iliondoa vikwazo vya matumizi ya dola na sarafu nyingine za kigeni mwaka huu kama njia ya kujaribu kuzuia kushuka kwa sarafu yake. IMF inafanya kazi kwa karibu na mamlaka ya Zambia kuendeleza mpango ambao utaimarisha uchumi wa taifa hilo.
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.

Share habari hii kadri uwezavyo.

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top