Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

RAIS MUTHARIKA AJIANDAA KUFUNGA NDOA SASA

Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.
Rais mpya wa Malawi Peter Mutharika anatarajiwa kufunga pingu za maisha na mpenzi wake wa muda mrefu,mwishoni mwa wiki. Taarifa hii ni kwa mujibu wa taarifa kutoka ikulu ya Rais.

Taarifa hiyo ilisema: ''Ikulu ya Rais ina furaha kuwajulisheini kuhusu harusi ya kitamaduni itakayofanywa kati ya Rais Arthur Peter Mutharika na mwandani wake wa muda mrefu Madam Gertrude Hendrina Maseko.''

Taarifa hii iliwasilishwa na msemaji wa Rais Chikondi Juma aliyesema kuwa sherehe ya harusi itakuwa ya faragha. Rais Mutharika aliibuka mshindi katika uchaguzi wa urais uliofanyika mwezi jana ambapo mshindani wake mkubwa alikuwa rais aliyeondoka mamlakani Joyce Banda. Rais Mutharika amewaambia maafisa wa serikali kuhakikisha kuwa hakuna pesa za serikali zitatumiwa katika shughuli hiyo.

Wa Mutharika ni Rais wa pili kufnya hasrusi akiwa mamlakani nchini Malawi
Mutharika, mwenye umri wa miaka 74 na ambaye mkewe alifariki , ana watoto watatu, wasichana wawili na mvulana mmoja. Baadhi ya wadadisi wanaunga mkono harusi ya Mutharika wakisema kuwa itasaidia kuimarisha maisha ya kijamii na kisiasa kama kiongozi wa nchi.

Hii ni mara ya pili kwa Rais kufanya harusi akiwa mamlakani nchini humo. Wa kwanza alikuwa Rais Bingu Wa Mutharika,aliyemuoa mpenzi wake Callista Chimombo, aliyekuwa waziri wa zamani wa utalii mwaka 2010. Wa Mutharika alikuwa nduguye mkubwa rais Peter Mutharika.

Hata hivyo wakosoaji wanalalamika kuwa pesa za umma zitatumika kwa harusi hii kwa sababu shirika la habari la taifa lilatumika kupeperusha matangazo ya harusi hiyo moja kwa moja. Pia wanasema kuwa Rais Mutharika atatumia rasilimali za serikali ikiwemo usalama wakati wa harusi yake ambayo wanasema bado ni gharama kwa serikali.
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.

Share habari hii kadri uwezavyo.

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top