Shirika la Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), limeendesha kambi za upimaji wa Afya Bure kwa wakazi wa Kanda ya Ziwa kwa kipindi cha mwezi mmoja.
Lengo la kambi hizi ni kuweza kutoa elimu na kuwahamasisha wanachama wa NSSF na wananchi kwa ujumla waweze kujenga tabia ya kupima afya zao mara kwa mara na kujiwekea mfumo bora wa maisha ili kuepukana na magonjwa sugu yasiyoambukiza.
Zoezi hili litaanzia mkoa wa Mara, Manispaa ya Musoma kwenye Viwanja vya Shule ya Msingi Mkendo, kuanzia tarehe 28/05/2014, kwa siku tatu mfululizo, kuanzia saa mbili asubuhi mpaka saa kumi na moja Jioni. Baadae, Kambi hizi zitaendelea katika mikoa ya Shinyanga , Wilaya ya Kahama, Mkoa wa Geita na Mkoa wa Kagera.
HUDUMA ZITAKAZOTOLEWA
Huduma mbalimbali zitatolewa bure kwenye kambi hizi zikiwemo;
Upimaji wa Shinikizo la damu
Upimaji wa sukari kwenye damu- Kisukari
Upimaji wa hali ya lishe (Uwiano wa Urefu kwa Unene)
Utoaji wa dawa za Minyoo Ushauri wa kitaalam kwa watakaokutwa na Matatizo Ushauri nasaha na upimaji hiari wa VVU (UKIMWI) Kutoa vipeperushi vya Maelezo ya uboreshaji wa Afya.
Huduma zote hizi zitatolewa na NSSF, BURE.
NSSF inaendelea kuwasii na kuwahimiza wakazi wa kanda ya ziwa kuwa waendelee kujiandikisha kwenye NSSF HIARI Scheme.
NSSF HIARI Scheme ni kwa ajili ya wajasiriamali wadogo, wachimbaji wadogo, Ushirika wa Bodaboda , Ushirika wa Wakulima pamoja na wanachama wa Mifuko mingine ya hifadhi ya jamii.
Jiunge na NSSF HIARI Scheme ili uweze kujipatia mafao bora ya NSSF yakiwemo Bima ya Afya BURE kwa familia nzima (SHIB), mikopo nafuu ya SACCOS, pamoja na Mafao bora mengineyo.
Wananchi wa kanda ya ziwa wanakumbushwa na kuhimizwa kujitokeza kwa wingi ili kupimwa na kupewa ushauri wa afya zao Bure.
NSSF INAJENGA MAISHA YAKO YA SASA NA YA BAADAE.
Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Jackson Msome ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa Kambi ya Upimaji Afya Bure Mkoani Mara akifafanua jambo mara baada ya kutembelea banda NSSF ambapo zoezi la upimaji afya lilikuwa likiendeshwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF). Watu 1080 walipima maambukizi ya virusi vya ukimwi na watu 2020 walipima magonjwa ya kawaida. Kulia ni Meneja wa Mafao ya Matibabu NSSF, Ali Mtulia.