Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

ASKARI 18 WAPONGEZWA KWA KAZI NZURI WANAYOIFANYA

Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.
Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe akimpongeza mmoja wa askari wa bandari ya Dar es Salaam, Cornel Kufahaidhuru katika hafla fupi ya kuwazawadia askari 18 wa mamlaka ya bandari Tanzania (TPA) kwa kazi nzuri ya kuimarisha ulinzi katika bandari hiyo jana jijini Dar es Salaam.

Serikali imetoa sifa kwa kitengo cha usalama cha Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) kwa kuimarisha ulinzi katika bandari na hivyo kuchangia kuifanya bandari hiyo kuongeza ufanisi. Akitoa zawadi kwa askari wa mamlaka hiyo walioonyesha moyo wa kujitolea na ufanisi jana jijini Dar es Salaam, Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe alisema kazi yao nzuri imeongeza usalama na kuvutia zaidi wateja.

“Ninawasifu kwa kazi nzuri mnayofanya,” alisema. Alielezea kuwa kujitolea kwao na ueledi wao umesaidia kuokoa mamilioni ya shilingi ambayo yangepotea kwa wizi katika bandari hiyo. Kutokana na kazi yao nzuri, Waziri alisema, sasa nchi mbalimbali zinaanza kuonyesha nia ya kutumia zaidi bandari hiyo kupitisha mizigo yao.

Akitoa mfano, Waziri huyo alisema ujumbe wa maafisa wa serikali ya Kongo na wafanyabiashara toka jimbo la Katanga waliotembelea bandari hiyo wiki hii ni ishara kubwa kuwa sasa bandari inaanza kurudisha heshima yake.

Baadhi ya zawadi zilizotolewa ni pamoja na pikipiki, televisheni, simu za mkononi, pesa taslim na kompyuta mpakato. “Natoa shukrani za dhati kwa wadau wote waliochangia zawadi hizi,” alisema Waziri. Takwimu zinaonyesha kuwa idadi ya meli zinazotumia bandari hiyo imeongezeka kutoka 1,236 mwaka 2011/12 hadi kufikia meli 1,301 mwaka 2012/13.

Kwa upande wa shehena mwaka 2012/13 bandari ilihudumia jumla ya tani milioni 12.5 ikilinganishwa na tani milioni 10.9 mwaka 2011/12, ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 15. Pia kwa mwaka wa 2012/13 bandari ilizihudumia nchi zinazotumia bandari hiyo shehena ya tani milioni nne ambayo ni sawa na asilimia 32 ya shehena yote.

Mwaka 2012/13 wastani wa Tshs bilioni 371.7 zilikusanywa, sawa na ongezeko la asilimia 14.3 ukilinganisha na Tsh. bilioni 325.3 mwaka 2011/12. Matukio ya uhalifu na wizi yamepungua kutoka matukio 21 mwaka 2011 hadi matukio 7 mwaka 2012, na kufikia matukio 3 mwaka 2013.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Madeni Kipande alisema juhudi za polisi hao wa mamlaka zimezaa matunda. “Ninatoa shukrani zangu kwa kitengo cha ulinzi na wafanyakazi wote kwa juhudi wanazoonyesha,” alisema.

Alimshukuru Waziri Mwakyembe kwa kuweka swala la usalama katika vipaumbele vya wizara. TPA iko chini ya wizara ya Uchukuzi. “Mamlaka itaendelea kutambua wafanyakazi bora na kuwapatia motisha,” alisema Kipande. Mkuu wa Kitengo cha usalama cha TPA, Bw. Lazaro Twanga alisema kutambuliwa huko kumewapatia motisha na nguvu ya kufanya kazi nzuri zaidi.

Hata hivyo, alisema swala la kuhakikisha usalama katika bandari hiyo ni la wafanyakazi wote na hivyo akataka ushirikiano wao. “Tushirikiane wote kuhakikisha bandari yetu inakuwa imara na yenye kuleta ushindani kwa faida ya taifa letu,” alisema.

Jiunge na mi kwa kubonyeza kwenye link zifuatazo chini ili kupata habari mpya zaidi. 
        FACEBOOK >>> TWITTER  >>> MATUKIO KWA NJIA YA SAUTI
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.

Share habari hii kadri uwezavyo.

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top