Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, ndugu Said Meck Sadick amefanya ziara ya ghafla katika soko la Mbagala mtaa wa kwa Mangaya leo hii.
katika ziala yake, amewaomba wafanya biashara wanao kaa katika maeneo jirani na soko hilo wajitokeze kwa wingi ili waweze kufanya soko hilo liendelee kukuwa na kuwasaidia wakazi wa maeneo hayo kwa ujumla wake.
Pia kiongozi huyo amewaomba wafanya biashara wote wanao fanyia kazi zao kandokando ya barabara, waache mara moja tabia hiyo na matokeo yake waamie kwenye soko hilo, ili waweze kunufaika na kuipenda zaidi kazi yao.
ila kwa upande wa wafanya biashara wa sokoni hapo pamoja na wanunuzi wa bidhaa mbalimbali kwenye soko hilo la mbagala kwa mangaya akiwemo mwana dada Mariam Chite wamesema kwa mba, tangu kufunguliwa kwa soko hilo, hakuna watu wakutosha wenye uwezo wa kujaza nafasi zilizo wazi ndani ya soko hilo, jambo ambalo linafanya kudorola kwa bidhaa na mpaka kupelekea watu kuamia sehemu nyingine zenye watu wengi.
Kwaiyo wanaiomba serikali iweze kuwasaidia kulitangaza soko hilo kwanza kisha na wanao watajitangaza kwa jinsi watakavyoweza, ili mwisho wasiku waweze kufanya biashara zao vizuri na zenye kuwa na faida zaidi.