Miaka ya nyuma ilikuwa Tajiri mwenye Basi akitaka kuajiri Dereva Swali la Msingi iliuweze kuajiariwa alikuwa anauliza kama Umewahi kuendesha gari wapi na ulikuwa ukitaja UDA kazi unapata haraka sana.
Tofauti na hali ilivyo sasahivi madereva wa uda wamekuwa hawana sifa kwani tunashuhudia wanavyo endesha hovyo magari hayo barabarani na pia hawaheshimu kabisa sheria na taratibu za uendeshaji wa vyombo vya moto.
Ni jana usiku tu tumeona moja ya gari hilo likiwa mtaroni kutokana na uzembe wa madereva hao,sasa na asubuhi ya leo tunaona basi lingine likiwa na tatizo hilo hilo huku wahusika wakiingia mitini.Je kuna nini kinaendelea nyuma ya pazia.