wa wagonjwa akiwa anangojea kupata huduma baada ya mvua hiyo kubwa kwisha .
Kila kitu kimekaa hovyo hovyo baada ya mvua kubwa hiyo kunyesha
Mapema mchana wa leo kumetokea mvua kubwa katika maeneo mbalimbali ya Jijini Dar es salaam kumesababisha usumbufu mkubwa baada ya maeneo mengi kukumbwa na tatizo la maji mengi ambayo yaliziba barabara , nyumba za watu pamoja na maeneo mbalimbali.
Mvua hizo kubwa ambazo hata mamlaka ya hali ya hewa wametahadhalisha kwamba zitakuwepo kuanzia Tarehe 5.03.2014 hadi Tarehe 7.03.2014 zimesababisha usumbufu mkubwa katika Hospitali ya Halmashauri ya Kinondoni Sinza - Palestina kujaa maji kila kona na kupelekea wauguzi kuacha kazi na kupanda juu ya Meza na viti wakikwepa maji hayo. Na wengine kukimbia katika eneo hilo kuhofia maji hayo.
Walikwepa maji hayo kutokana na kwamba si ya mvua tuu lakini yalikuwa ni Machafu yaliyochanganyikana na maji kutoka vyooni ambapo kuna chemba moja ya maji machafu imepita hapo.
Baada ya mvua hiyo kwisha iliwalazimu wafanya usafi wachukue muda wa zaidi ya dakika 30 kufanya usafi na kutoa matope yaliyokuwa yamejaa kila chumba.
Akiongea kwa Simu Mganga Mkuu wa Hospitalu hiyo amekili kwamba kuna usumbufu mkubwa wa chemba hiyo na mvua hasa katika kipindi hicho ambapo zinanyesha kwa kiasi kikubwa.
Ameongeza kwa kusema kwamba kunajuhudi zinahitajika kufanyika ili kuweza kunusuru tatizo hilo lisiendelee.
Nao baadhi ya wagonjwa ambao wengine walikuwa katika hali ambayo si nzuri wamesema wanaiomba serikali itazame tatizo hilo maana licha ya maji hayo kuwa mengi lakini pia ni hatari kwa afya zao kwa ujumla.