Jee ni kwa nini ccm mara nyingi inajenga chuki zidi ya watu wenye asili ya Pemba ? au Pemba si sehemu ya Tanzania Mh Kikwete?
Takribani nimechunguza katika hutuba nyingi za ccm navitendo vingi vinavyotokea Visiwani Zanzibar walengwa wakubwa ni watu wenye asili ya Pemba , hata kufikia hadi 1995 kuvunjwa Nyumba za watu wenye asili ya Pemba kwa chuki tu za kibaguzi na kisiasa .
Sasa mambo haya nilizani yako Zanzibar tu, Lakini tulisibitisha kumuona Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Watu wa Tanzania Mh Jakaya Mrisho Kikwete bila kutafuna maneno au kumuonelea aibu Msaidizi wake Raisi wa Zanzibar Ali Mohammed Shein na Makamo wa kwanza wa Raisi wa Zanzibar Maalim Seif Shariffu Hamadi na viongozi mbali mbali wenye asili ya ?.
Alitumia maneno ya ubaguzi na vitisho kama vile watu Wenye asili ya Pemba hawana haki ya kuishi na kukaa Tanzania .
Kwa Mtazamo huu na Baraka alizozitoa Raisi ikiwa kama mlezi wa Wananchi wote wa Tanzania bila kujali rangi asili au wapi unatoka , huu ni ubaguzi mkubwa kwa mtu kama yeye na nihatari kuliangamiza taifa kwa kutumia kwa chuki za kibaguzi kama hizi za kutaja hazarani jamii fulani kuendelea vitendo hivi vya kibaguzi kwa watu wenye kuonekana wana asili ya pemba.
Sisi Watu Wenye asili ya Pemba tunalani sana kitendo hichi cha Raisi wa nchi ambaye ni mlezi wa nchi kua si chakiungwana hata kidogo kwa vile hakikumlenga mtu moja au chama cha siasa kimelenga yamii mzima na tabaka fulani katika nchi hii.
Tumezoea kuona chama chake akiwa yeye ni Mwenye Kiti Taifa na Raisi wa Nchi hii kwa upande wa Zanzibar kila wanapopata fursa fulani , hutumia kigezo hichi cha ubaguzi kama vile ni mtaji wa chama chao kukiimaricha zidi ya kuwatukana watu wa jamii fulani (Wapemba) na bila kukemea kwa ubaguzi huu unao lenga jamii mzima na si chama cha siasa au kikundi fulani.
Huu umekua ni kama yale mauwaji ya Kimbari tunayo yalani Watanzania zidi ya Wahutu na Watusi.
Hatua hii akiwa Mh Rais Kikwete hato omba Razi Basi inaweza kuleta mfarakano na vita vya ubaguzi .
Lakini kitendo hichi cha Raisi wa Jamuhuri ya watu wa Tanzania kimetusikitisha zaidi kwa mtu kama yeye na wazifa wake alonao kubagua watu wa asili hii bila kujali kua yeye ni kama Baba kwenye Nyumba na kuleta ubaguzi kwa badhi ya watoto wake.
Hili ni jambo tunalilani na nikupandikiza chuki zidi ya watu wenye asili ya Pemba na kuonekana ni watu wasio na haki Tanzania ,tunaweza kutafsiri kuona huu ni mkakati na ilani ambayo inapata baraka hata na viongozi wa kitaifa akiwemo kiongozi wa nchi Raisi Kikwete.
Sasa tumebaini kuwa hawa uvccm Zanzibar kufanya vitendo vya uvunjaji wa Sheria na kuwatukana watu wenye asili ya Pemba, ni Baraka za viongozi wao wa juu .
Ikiwa Pemba si Sehemu ya Utawala wake Kikwete kwa chuki kama hizi basi nibora kukitengua kisiwa Cha Pemba na Wapemba wakawa kivyao.
Nawakilisha kwa Niaba ya Wapemba wenzangu Makame Silima
M/mungu tulinde na utukinge na wabaya wote na uibariki Zanzibar na Tanzania yote.