Karibu tena ndugu mdau katika kona ya afya. Leo tuta angazia juu ya umuhimu na faida zitokanazo na zao la Tende.
Tende ina faida kubwa katika miili yetu na ni Muhimu sana kuitumia, miongoni mwa faida hizo ni pamoja na:
1- Kwa watu wenye matatizo ya tumbo, nicotinic inayopatikana kwenye tende husaidia kurekebisha matatizo ya tumbo na huleta ahueni kwa watu wenye matatizo ya kupata choo.
2- Tende husaidia kuuimarisha moyo. Iloweke tende kwenye maji kwa usiku mmoja na asubuhi kunywa maji hayo pamoja na tende zilizolewekwa baada ya kuondoa mbegu, ukifanya hivyo mara mbili kwa wiki, moyo wako utakuwa imara.
3. Utafiti umeonyesha kuwa tende husaidia kutanua misuli ya mji wa mimba wakati mwanamke anapokaribia kujifungua, hii husaidia kumfanya mwanamke asipoteze damu nyingi wakati wa kujifungua.
4- Wataalamu wa vyakula, wanazichukulia tende kama chakula bora kwa wanawake wanaonyonyesha kwani husaidia kuyapa maziwa virutubisho muhimu vinavyomfanya mtoto awe na afya njema.
5. Husaidia mlaji kuongeza protini na Vitamin B1,B2,B5,A1 na C,hivi ni muhimu kwa usatawi wa mwili wa binadamu.
6 .Huimarisha na kuboresha mfumo wa usagaji chakula tumboni,hivyo mlaji ataondokana na tatizo la ukosefu wa choo,au kupata choo kigumu.
7. Tende hufanya mwili kuwa na nguvu na kuondoa uchovu, kwa sababu tende ina sukari asilia,ndani ya nusu saa tu uchovu unaondoka,hii ni kwa sababu ya glucose,ukitaka ufaidi zaidi changanya na maziwa fresh, so badala ya kunywa vinywaj baridi kama vile Redbull au malta kula tende.
8. Tende huimarisha mishipa ya fahamu kwa sababu ina madini ya chumvi kidogo na potashiamu.
9. Kwa wenye matatizo ya upungufu wa damu mwilini wanashauriwa kula tende wanaweza kupata ahuweni, pia tende huzuia uozaji wa meno tofauti na vitu vingine vitamu
10.Tende zina nafasi yake kwenye kuongeza NGUVU ZA KIUME, mchanganyiko maalum wa tende, maziwa, asali na unga wa hiriki huondoa tatizo hili
11.Tende inatibu saratani ya TUMBO, inafanya kazi vizuri kuliko dawa ya kizungu.
12- Kutokana na madini ya chuma kwenye tende, watu wenye upungufu wa damu hupata ahueni.
13- Vitamin B1 na B2 vilivyopo kwenye tende husaidia kuyapa nguvu maini.
14- Tende pia huleta ahueni kwa watu wenye kikohozi na mafua.
15. Tende husaidia pia kwa mke na mume. Iloweke tende kwenye maziwa ya mbuzi usiku, asubuhi changanya maziwa hayo na asali kisha kunywa, njia hii husaidia kuongeza nguvu na stamina za kufanya mapenzi.
16. Tende husaidia kuchelewesha dalili za uzee na pia husaidia kurekebisha ngozi na huondoa mabaka ya kuungua na jua.
''Ama hakika tende ndio tunda pekee lenye kuupatia mwili vitu vinne kwa wakati mmoja, vitamin, protini, wanga na mafuta'' Tende inatibu saratani ya tumbo.
Habari njema kuhusu tende kama tiba ni kwamba, haina madhara yoyote kwa sababu ni dawa asilia na inafanyakazi vizuri kuliko dawa za ‘kizungu’. Tende vile vile ina imarisha nuru ya macho na tatizo la kutokuona usiku (night blindness).
Kwa ujumla faida za tende ni nyingi na unaweza kuila tende kwa namna mbalimbali, kama vile kuchanganya na maziwa, kuchanganya na mkate au vitafunwa vingine. Ifanye tende kuwa sehemu ya mlo wako wa kila siku ili ujipatie faida hizo. Kumbuka kutumia zao hili la tende japo mara tatu kwa mwezi.