Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

Tumia matunda kujitibu makovu ya mwili.

Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.
Uwepo wa mabaka na madoa usoni ni tatizo linalowakabili watu wengi na kuwafanya kuhangaika huku na kule kutafuta dawa ili kukabiliana nalo, lakini hujikuta wakiishia kutumia vipodozi vyenye kemikali ambavyo huishia kuharibu ngozi za wengi wao.Zipo njia mbalimbali za asili, zinazoweza kukabiliana na tatizo hili ikiwamo matumizi ya papai.Wengi tumekuwa na fikra kuwa papai ni tunda linalofaa kuliwa na kutengenezwa juisi tu bila kufahamu kuwa lina matumizi makubwa zaidi ya hayo.

Ukweli ni kwamba, licha ya papai kuwa ni tunda lenye umuhimu mkubwa katika mwili wa binadamu linapoliwa au kunywa juisi yake, pia linaweza kutumika kama dawa au kinga katika ngozi na kuifanya ionekane yenye mvuto wakati wote.Papai pia lina uwezo wa kuondoa madoa yanayowasumbua wengi katika ngozi hasa usoni na kuiacha ngozi iking’ara.

Mchanganyiko wa papai na asali ni tiba nzuri kwa maradhi ya ngozi ukilinganishwa na matumizi ya vipodozi vingine vyenye kemikali.Njia nyingine inayoweza kusaidia kuondoa mabaka na madoa mwilini ni majani ya alovera. Majani haya yanapaswa kupakwa na kusugua eneo liloloathirika, utomvu wake husaidia kufuta mabaka hayo.

Jinsi ya kufanyaSafisha uso kwa maji ya uvuguvugu kuondoa taka zote zilizopo, kisha kausha vizuri kwa kitambaa kikavu.Katakata papai katika vipande vidogovidogo, visage kwa kutumia mashine au twanga katika kinu mpaka vilainike kabisa na upate rojorojo.

Changanya rojo uliyopata na asali, kisha endelea kukoroga hadi vichanganyike kabisa.Paka mchanganyiko huo usoni, kaa nao kwa muda wa dakika 15 hadi 20, kisha safisha uso.Kama utatumia alovera, fuata pia hatua hizi, huku ukisugua katika maeneo yote yaliyoathirika mwilini.

Safisha uso kwa maji ya uvuguvugu kuondoa taka zote zilizopo, kisha kausha vizuri kwa kitambaa kikavu. Fanya hivyo mara mbili kwa siku kwa muda wa mwezi mmoja, utaona mabadiliko katika ngozi ya uso na madoa yote yatafutika nakuisha kabisa.
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.

Share habari hii kadri uwezavyo.

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top