Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

Serikali yatoa ufafanuzi juu ya vitambulisho vya waandishi wa habari.

Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.
SERIKALI imetoa ufafanuzi juu ya vitambulisho vya waandishi wa habari
( Press card) wakati wa Bunge Maalum la katiba na kusema kuwa ndicho kigezo pekee  kitakachowezesha  waandishi wa habari kutimiza majukumu yao vyema katika kipindi  chote cha bunge hilo.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam  na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Assah Mwambene wakati akitoa tamko la Serikali kufuatia  taarifa potofu zilizoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari hapa  nchini.

Mwambene alibainisha kuwa  utaratibu wa kutoa vitambulisho hivyo si  mgeni kama ilivyodaiwa na baadhi ya vyombo vya habari na kwamba unaweza kukipata ndani ya saa 24 ikiwa tu mwandishi anakidhi vigezo. 

Alisema vitambulisho vinatolewa tu kwa mwandishi mwenye taaluma ya uandishi wa habari kutoka chuo kinachotambulika naSerikali kwa kuzingatia sheria na kanuani zilizowekwa.Alisisitiza  kuwa utaratibu wa kutoa  vitambulisho kwa waandishi  habari upo  na ni wa kisheria  hivyo ni lazima ufuatwe. 

Pia  alisema kuwa ni vyema kila mwandishi akafuata taratibu zote za kupata kitambulisho kinachotolewa na MAELEZO kwa kuwa bila kitambulisho hicho hataweza kufanya kazi  katika kazi rasmi kama vile Bunge maalum la katiba.

Alitoa wito kwa waandishi wa habari kujiendeleza katika taaluma ya uandishi wa habari kwa wale wasio na sifa za kupewa vitambulisho hivyo ili kuiniua Sekta ya Habari hapa nchini.

Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.

Share habari hii kadri uwezavyo.

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top