Kwa muda mrefu kumekuwa na tetesi za mastaa wa muziki Drake na Rihanna kwamba wamerudisha uhusiano wao wa kimapenzi.Ingawa wawili hao waliopachikwa jina la ‘AubRih’ (Kwa maana ya Aubrey na Rihanna) mpaka sasa wamekuwa wakisisitiza bado ni marafiki wa kawaida, headlines zao za hivi karibuni zinaonyesha kuna kitu zaidi ya urafiki kati yao.
Rihanna amekuwa akionekana na Drake wakiongozana kwenye ziara ya kimuziki ya Drake Ulaya ambapo kwa mara ya kwanza walionekana pamoja nchini Ufaransa, kisha Ujerumani na jana usiku walionekana pamoja jijini Manchester – England.
Na hizi ni picha za ushahidi wa wawili hao walivyokuwa wakijiachia kwenye mitaa ya jiji la Manchester usiku jana.Drake na Rihanna kwenye mitaa ya Manchester jana usiku. samahani kwa kutoweza kuonesha picha tajwa hapo juu kwa sababu zilizopo juu ya uwezo wetu kiteknolojia. khali ikiwa shwali utaziona.