Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

Mke wa mtu hatari.

Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.
Issa Mnally Na Richard BukosKIJANA mmoja mtanashati ‘Sharobaro’ ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja juzikati alijikuta akichezea kichapo cha mbwa mwizi kisa kikidaiwa kuwa ni mke wa mtu.

Tukio hilo lilijiri saa saba usiku mwishoni mwa wiki iliyopita, Chalinze mkoani Pwani ambapo mapaparazi wetu walikwenda kwa ajili ya uzinduzi wa kundi jipya la sanaa liitwalo 3 Ways.Wakati shamrashamra zikiendelea, ghafla liliibuka timbwili na katika kufuatilia ilibainika sharobaro anayeishi eneo hilo alikuwa akila kipigo kutoka kwa mwanaume mmoja akimtuhumu kuwa alimkuta akiwa amekaa chobingo kihasarahasara na mkewe.

Licha ya baadhi ya wasanii kujaribu kuingilia kati ugomvi huo, jamaa huyo aliendelea kushusha kichapo hadi pale watu walipomtolea uvivu na kumzuia asije akasababisha mauaji.“Unajifanya sharobaro halafu unazengea wake za watu, sasa wee umeipata fresh na huyo mwenzako akirudi nyumbani nayeatakiona,” alisikika akisema mwanaume huyo huku akionekana kufura.

Kufuatia kichapo hicho, sharobaro huyo alijikuta akiangua kilio huku akilalama kuwa mwanamke huyo amemponza na kumharibia siku yakeWakizungumzia tukio hilo, baadhi ya mashuhuda walisema, kipigo alichopata kijana huyo ni fundisho kwa masharobaro wengine ambao wamekuwa na uhusiano wa karibu na wake za watu.

“Unajua hawa vijana hii ndiyo dawa yao, wanajisahau sana. Yaani anajua kabisa fulani ni mke wa mtu lakini anajiweka, sasa kwa kipigo hiki atakuwa fundisho,” alisema baba mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Baba Zulfa.Aidha, wengine walimtetea kijana huyo na kudai kuwa mwanamke huyo ndiye anayestahili kulaumiwa kwa kukubali kukaa gizani na kijana huyo wakati akijua ni mke wa mtu.
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.

Share habari hii kadri uwezavyo.

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top